Rihanna Apigwa Marufuku Kuingia Nchini Senegal
Mwanamuziki wa kimataifa Rihanna anategemewa kuhudhuria mkutano mkubwa nchini Senegal,lakini vikundi vya dini nchini humo wamekataa kumpokea, chombo cha habari cha Jeune Afrique kimeripoti.
"Tumeukataa ufreemason na mapenzi ya jinsia moja" , shirika la vikundi 30 vya kidini wamesema, wakimshutumu mwaimbaji huyo kwa kutumia ishara za freemason na kuwa mjumbe wa chimbuko la Illuminati , lilanoaminika kuwa ni kundi maalum la watu ambao hudhibit masuala na uongozi wa dunia na inasadikika kuwa hufanya shughuli zao kisiri kudhibiti kila kitu na kuunda Utawala Mpya wa Dunia.
Shutuma hizo zimefutiliwa mbali na wasanii waliowahi kufanya nao kazi huko nyuma,
Rihanna atatembelea nchi hiyo ya Afrika Magharibi akiwa kama balozi wa shirika la elimu 'Global Partnership Foundation'
Shirika hilo lina lengo la kuchangisha fedha za kusomeshea mamilioni ya watoto na vijana katika nchi zinazoendelea.
Chombo cha habari cha Jeune Afrique kimemnukuu Waziri wa Mambo ya Ndani akisema kuwa atahakikishia usalama washirika wote wa mkutano huo.
No comments