Header Ads

NIGERIA Kumpa Heshima Anthony Joshua, Siku chache baada ya kumbonda Klitschko kwa K.O



Baada ya kumuangusha bondia kutoka Ukrain Wladimir Klitschko, Serikali ya jimbo la Ogun nchini Nigeria ambapo ndipo walipokulia wazazi wa Anthony Joshua inajiandaa kumtunuku mkali huyo wa masumbwi.

Yinka Mafe, ambae ni kiongozi katika jimbo hilo anasema watabadili jina la uwanja wa Sagamu na kuuita jina la bondia huyo vile vile watabadili jina la mtaa maarufu jimboni hapo "Cinema Street" kuitwa Anthony Joshua Street, ambao nusu yake unamilikiwa na familia ya Joshua.

Hata hivyo barabara za mtaa huo zilijengwa katika miaka ya 50 na babu yake Anthony, Omo-oba Daniel Adebambo Joshua, moja kati ya miundo mbinu ya kale ya nchini Nigeria.

Mafe pamoja na mamia ya wakaz wa Sagamu waliungana kutazama mpambano wake.


"Tunafurahia mafanikio yake, ni mwana Sagamu, na tutakua na furaha kuonyesha jinsi tunavyojisikia"



Picha zaidi kutoka Kwenye Mpambano wa Anthony Joshua Na Vladmir Klitchko Kwenye Dimba La Wembley London Uingereza







No comments

Powered by Blogger.