Header Ads

Mwanaume Mmoja Nchini Zimbabwe Ajibadili kuwa mwanamke ili kumfanyia mtihani mpenzi wake

.
Mapenzi Yakikolea Mtu Yuko Radhi Kufanya Jambo Lolote Ili Kumfurahisha Mpenzi Wake Na Ndio Maana Watu Wakasema Mapenzi Yana "Run" Dunia, Tukio Moja la kustaajabisha Limetokea Nchini Zimbabwe Ambapo  Mwanaume Mmoja amekamatwa kwa kujaribu kutaka kumfanyia  mtihani wa sekondari mpenzi wake.

Mtu huyo alivalia mavazi ya kike na kuweka nywele bandia pamoja na kupaka rangi mdomo ili kufanana na   mwanamke

Kwa mujibu wa mtandao Mmoja Wa Nigeria  Naija.com mwanaume huyo alikamatwa katika chumba cha mtihani alipokuwa akijaribu kufanya mtihani huo katika shule moja iliyopo nchini Zimbabwe, ambapo wasimamizi wa chumba hicho cha mtihani walimtilia shaka na kuanza  kumkagua.
Moja ya wasimamizi hao amesema kuwa mwanaume huyo amefikishwa katika vyombo vya ulinzi kwa mahojiano maalum.

 

1 comment:

Powered by Blogger.