Mtu Mmoja Nchini Msumbiji Alazimishwa Kuoa Maiti
Mtu mmoja kusini mwa Msumbiji katika mkoa wa Inhambane
alilazimika kumlipia mahari mkewe aliyefariki wikendi iliopita kwa Mujibu wa chombo cha habari cha taifa.
Baada ya mkewe kufariki kutokana na matatizo ya kujifungua
,ndugu zake walimlazimisha mwanaume huyo kulipa ''Lobolo' (Mahari)', la sivyo hakuna kuzika mwili wa marehemu.
Ndugu zake walimshutumu kijana huyo kwa kushindwa kuafikia
majukumu yake ikiwemo kutambulishwa kwa jamaa na ndugu za mwanamke huyo kabla
ya janga hilo kutokea.
Ili kuhakikisha kuwa mazishi hayo yanafanyika, kijana huyo
alilazimika kumnunulia nguo na viatu mkewe aliyefariki, kisha kukubali kulipa zaidi
ya dola 800 na kufunga harusi.
Ndugu mmoja wa kijana huyo aitwae Irmao do Jovem alielezea kuwa.
''Tulijaribu kuchangisha fedha walizotaka, lakini tuliweza
kuchangisha dola 178 pekee.Hivyobasi ilibidi kuweka ahadi ya kulipa fedha
zilizosalia siku ya harusi''.
Huku ikiwa familia ya kijana huyo imekubali
kulipa,walishutumu tabia ya familia ya mwanamke huyo.
Hatahivyo, ni utamaduni miongoni mwa makabila mengi nchini
Mozambique hususan iwapo mwanamume anaamua kuishi na mwanamke bila kufuatilia
utamaduni wa kumuoa mwanamke huyo.
No comments