Ni Marufuku Kuvaa Jezi Ya Barcelona Saudi Arabia Ukikutwa Jela Miaka 15
Kwa Mujibu Wa mtandao Maarufu wa dailymail.co.uk wa Uingereza, Ni marufuku kuvaa jezi ya FC Barcelona imefungiwa nchini Saudi Arabia na
ukikutwa umevaa unaweza kufungwa.
Jezi ya FC Barcelona yenye
nembo ya Qatar Airways imefungiwa kuvaliwa na watu Saudi
Arabia na ikitokea umevaa unaweza kupigwa faini ya pound 120,000
ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 300 na kifungo cha miaka 15 jela.
Jezi za Barcelona ambazo zina logo ya Qatar
Airways ambao wamekuwa wadhamini wao katika kipindi cha miaka minne
iliyopita, Saudi Arabia inaripotiwa kuwa logo ya Qatar Airways ipo nje kisheria
au kinyume na taratibu, hivyo ukikutwa utakutana na adhabu ya kifungo.
Habari Njema ni kwamba FC Barcelona wataanza kuvaa jezi zikiwa na mdhamini wao mpya Rakuten kuanzia msimu ujao wa 2017/18 hivyo mashabiki wa FC Barcelona nchini Saudi
Arabia watakuwa na nafasi ya kuvaa jezi za timu yao zenye logo ya Rakuten na
sio ya Qatar Airways.
No comments