Eminem ashtaki chama tawala cha New Zealand
Mwanamuziki
mashuhuri Eminem amekishtaki chama tawala cha New Zealand kuhusiana na wimbo
wake ambao umetumiwa kwenye tangazo la kampeni.
Rapa huyo
amesema wimbo uliotumiwa katika tangazo la chama cha National Party mwaka 2014
ulikuwa makala ambayo haikuwa imeidhinishwa ya wimbo wake wa Lose Yourself.
Lakini
mawakili wa chama hicho wanasema wimbo uliotumiwa haukuwa wa Lose Yourself,
bali ni wimbo ufahamikao kama Eminem-esque ambao waliununua kupitia soko la
jumla la muziki mtandaoni.
Kesi hiyo
ilianza Jumatatu, ambapo nyimbo zote mbili zilichezwa katika ukumbi wa
mahakama.
Wakili wa
Eight Mile Style, kampuni inayomuwakilisha mwanamuziki huyo, amesema wimbo wa
Lose Yourself ulikuwa na kipekee na bila shaka ni fahari ya kazi za sanaa za
Eminem.
Tangazo hilo
la mwaka 2014 lilikuwa na picha za wapiga makasia na sauti nyuma yake
ikiwahimiza watu kudumisha "timu ambayo inafanya kazi" na kurejesha
National Party madarakani katika uchaguzi uliokuwa unakaribia.
Wimbo
uliotumiwa, Eminem-esque, unakaribiana sana na Lose Yourself, ambayo ulitumiwa
katika filamu ya Eminem ya 8 Mile ambayo ilitolewa 2002.
Nyimbo ambazo
hukaribiana sana na nyimbo halisi ambazo ni maarufu sana, lakini zina tofauti
kidogo vya kutosha kutokiuka sheria ya hakimiliki, mara kwa mara huwekwa kwenye
masoko ya pamoja ya nyimbo zilizo huru kutumiwa.
Lakini wakili
wa Eight Mile Style Gary Williams amesema matumizi ya wimbo huo ulikuwa ni
ukiukaji wa sheria ya hakimiliki.
No comments