Kilichojiri Kwenye Siku Ya Mwisho Ya Dirisha Dogo la Usajili Barani Ulaya
Siku Ya Mwisho ya usajili ni siku amabayo wachezaji wengi wanahama sana kutoka timu moja kwenda timu nyingine, Jana ilikuwa ni siku ambayo wachezaji wengi wamehamia timu mpya ili kusaka changamoto mpya kwenye vilabu vyao vipya
1. Pierre Emerick Aubameyang
Aubameyang kutoka Borussia Dortmund Kwenda arsenal Arsenal kwa dili la Paundi Million 56 kwa mkataba wa muda mrefu.
2. Olivier Giroud;
Klabu Ya Soka Ya Arsenal Imeuza Jumla Ya wachezaji wanne katika dirisha hili la usajili amabao ni Theo Walcott, Francis Coquelin, Alexis sanchez na Olivier Giroud aliyejiunga na mahasimu wao Chelsea kwenye siku ya mwisho ya usajili hapo jana kwa dau la paundi million 18 na amesaini mkataba wa miezi 18 kuitumikia klabu hiyo yenye maskani yake pale Stamford Bridge
3. Michy Batshuayi;
Mchezaji wa kimataifa kutoka ubelgiji anayekipiga katika klabu ya chelsea Michy Batshuayi Anetimkia Kwenye klabu ya Borussia Dortmund kwa mkopo kuziba pengo la Aubameyang aliyetimkia Arsenal
4. Lucas Moura Atua Tottenham Hotspurs; Kiungo huyo amekamilisha usajili jana akitokea klabu ya soka ya PSG na Kutua Jijini London kwa Dau la Paund million 25
Baadhi Ya wachezaji Wengine waliohama ni:-
Eliquilam Mangala Kutoka Manchester City Kwenda Everton Kwa Mkopo
Jordan Hugil kutoka Preston kwenda West Ham United
Andy King Kutoka Leicester city Kwenda Swansea Kwa Mkopo
Slimani Kutoka Leicester city Kwenda Newcastle United
Mitrovic Kutoka Newcastle kwenda Fulham Kwa Mkopo
Alexander Soloth Kutoka Midtjylland Kwenda Crystal Palace
Martin Dubravka Kutoka Sporting Prague kwenda Newcastle United
Badou Ndiaye Kutoka Galatasaray Kwenda Stoke City
No comments