KABILA LA AZTEC NA KAFARA ZA AJABU.
Kiufupi wao waliamini kila ifikapo asubuhi mungu wa jua huamka na kufukuza giza lote pamoja nyota na mwezi na hivyo kuondoa nguvu zote za giza na kuleta mwanga.Pia waliamini Mungu huyu huwa anachoka sana ifikapo jioni na hivyo huenda kupumzika, in which case nguvu za giza,nyota na mwezi hurudi.Pia waliamini ili Mungu huyu aweze kurejesha nguvu mwilini ili aendelee na kazi kesho yake asubuhi, anahitaji apatiwe lita za kutosha za damu ya binadamu, pia ilibidi apewe mioyo ya binadamu kama kisusio cha kumpa nguvu za ziada.Ili kupata damu na mioyo hiyo, wa-Aztec walivamia vijiji vya jirani na kuteka 'makafara' maelfu kwa maelfu, waliwaongoza kwa misururu iliyoweza kufikia urefu wa kilometa kadhaa kuelekea kwenye pyramid la kafara lililopo mjini(now mexico city) ndani ya aztec. Wanapofika hapo huwa wanapandishwa kwa makundi hadi kileleni ambako kwanza wanapigwa kisu cha kifua na kuraruriwa wakiwa hai, baada ya kifua kufumuliwa na kabla hajakata roho, moyo hung'olewa kwa mkono wa kulia wa mkuu wa ibada 'high priest', na wakati anatapatapa kichwa chake hufyekwa kwa panga kali ambapo kichwa hubingilika hadi chini na damu kumwagika kuelekea chini, hii ni ili tu kumpa nguvu mungu jua.Haya yote yalifanyika huku 'makafara' wengine wakitazama 'live' kwa macho yao huku wakisubiri zamu yao ya 'ku-kafiriwa' kwa mungu jua. Ni tukio lililoweza kuchukua hadi siku 4 amabapo hadi 'makafara' 50,000 walitolewa kafara kwa kwa mwaka mmoja.
××××××××××××××××××××××××××××××××××
usikose mwendelezo
SHARE NA SAMBAZA..
No comments