Header Ads

NEYMAR AANZA VITIMBI

STAA wa Brazil,Neymar Jr ni kama ameamua kulazimisha kuondoka kwa nguvu katika klabu yake ya Barcelona hii ni baada ya leo kuchapana makonde mazoezini na beki mpya wa klabu hiyo Mreno, Nélson Semedo aliyesajiliwa hivi karibuni kutokea Benfica.
Picha za video kutoka eneo la tukio zimemuonyesha Neymar Jr anayewindwa na PSG akimvamia Semedo na kuanza kurushiana nae makonde kwa sekunde chache kabla ya wachezaji wenzao kuingilia kati na kuwaamua.Chanzo cha kutupiana makonde ni kuchezeana rafu.
Baada ya kuwaamua Neymar alivua kivazi cha kufanyia mazoezi (Bib) na kukitupa chini kisha akapiga mpira kwa hasira golini na kuondoka zake kabla ya mazoezi kumalizika.
Kwa sasa Barcelona iko Miami,Marekani ikijifua kujiwinda na mchezo wake wa kesho Jumamosi dhidi ya wapinzani wao wakubwa,Real Madrid.


No comments

Powered by Blogger.