Header Ads

HIZI NDIZO NCHI AMBAZO RAIA WAKE HUISHI KWA MIAKA MINGI

Image result for enjoying life

Siku zote mwanadamu hapendi kifo. Katika kuhakikisha anaendelea kuishi, hupambana kwa kila hali ili aendelee kubaki salama. Miongoni mwa njia zinazotumiwa kujihakikishia miaka mingi ya kuishi, ni kufanya mazoezi na kula vizuri. Hayo ndiyo yafanywayo na watu duniani kote. Pamoja na harakati zote hizo, yapo mataifa ambayo kwa wastani watu wake huishi miaka mingi zaidi ukilinganisha na mataifa mengine. Katika orodha hii ya nchi nne ambazo watu wake huishi miaka mingi, zipo siri zinazofanya waweze kudumu kwa muda mrefu:

JAPAN
Wanaishi kwa wastani wa miaka 83. Sababu kubwa inayotajwa kuchangia katika kusogeza umri ni vyakula vya jadi wanavyokula. Viazi vitamu na samaki ni aina ya vyakula vyenye mchango mkubwa. Pia, jamii imara isiyo na migogoro mingi inawasaidia kupunguza msongo wa mawazo.

HISPANIA
Wastani wa kuishi ni miaka 82.8. Siri kubwa ya kuufikia umri huu ni utajiri wa mafuta bora kwa afya ya mwanadamu (Olive Oil) na ulaji wa mboga za majani kwa kiasi kikubwa. Jambo jingine lisilopaswa kusahaulika, ni tabia ya wakazi wa nchi hii kupendelea kutembea zaidi na kuendesha baiskeli hata kama wana magari.

USWISI
Ni mojawapo ya nchi tajiri Ulaya. Raia wa nchi hii wanaishi kwa wastani wa miaka 81. Wamefanikiwa kufikia wastani huo mkubwa kwa sababu ya huduma bora za afya, usalama wa raia na mali zao na upendo uliotapakaa katika viunga vya nchi hii tajiri.

KOREA KUSINI
Tafiti za hivi karibuni zinaitaja kuwa nchi ya kwanza kwa raia wake kuishi miaka mingi. Wana wastani wa miaka 90! Wamefikia wastani huo kwa kupendelea kula vyakula vilivyochachishwa ambayo inasemekana vinasaidia kupunguza mafuta mwilini, kuongeza kinga ya mwili, na kuzuia kansa. Pia vyakula vya Wakorea vina kiwango kikubwa cha ufumwele (fibre).

VIPI KUHUSU TANZANIA?
Tunaweza kuongeza wastani wa siku zetu za kuishi endapo tutazingatia haya: Ulaji wa vyakula bora, kufanya mazoezi, ulinzi wa watu na mali zao na uboreshaji wa huduma za kiafya. Mambo haya na mengine ambayo hayakutajwa, yaende sambamba na ukuzaji wa pato la kila mtu.

No comments

Powered by Blogger.