Header Ads

Wema Sepetu Aingia Rasmi Kwenye Muziki


Maisha na muziki ilikuwa ni moja ya vibwagizo maarufu sana kwenye wimbo wa muziki wa darassa. Sasa habari mpya mtaani kwa sasa ni kwamba msanii wa filamu na maigizo, ama bongo movies kama ilivizoeleka Wema Issac Sepetu ama Sepenga kama anavofahamika na baadhi ya watu kaamua kuingia kwenye tasnia ya muziki

Akiwa katika interview na planet bongo ya East Africa radio producer wa MJ Records Daxo Chali amethibitisha hilo.

Producer Daxo Chali ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa Wema Sepetu ameshiriksha katika wimbo wa Haitham ambao utatambulishwa siku ya jumamosi

Daxo pia amemsifia wema kuwa ni msanii mzuri na anajua kuimba vizur pia,Daxo pia ameongezea kuwa haitham ameamua kumshirikisha wema kuondoa ile kasumba iliyokuwepo kuwa wimbo wake wa mwanzo alibebwa na Mwana FA

Mwanzo wimbo huo ulipangwa aimbe Haitham peke yake lakini akatoa wazo la kumtafuta Wema na kumshirikisha  katika wimbo huo na apo Wema akarafutwa na kuingiza sauti kweny wimbo huo.

“Kuna siku kweli akaja, so tukamuingiza studio tukamuonyesha mashairi aingize wala hakusumbua, kwanza Wema anajua kuimba sema watu wengi hawajui ilo suala ila kitu kilichokuwa kinamsumbua sana ni zile melodi kwa sababu ile ngoma ni ya kiswahili lakini imeimbwa kama kifaransa, so ndio kitu kilichokuwa kinamsumbua sana ni kutamka yale maneno lakini kwenye kukaa kwenye key yupo vizuri sana,” amesema Daxo.

No comments

Powered by Blogger.