Header Ads

Lionel Messi Afunga Pingu Za Maisha Na Mama Watoto Wake



Usiku wa kuamkia leo nyota wa Barcelona Lionel Messi amefunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Antonella Roccuzzo.

Ndoa hiyo imefungwa mjini Rosario,Kaskazini mwa Argentina ambapo wawili hao wamekua pamoja.

Wawili hao ambao wamekuwa katika mahusiano kwa miaka 25, walizuia mtu yoyote kuja na simu katika hafla hiyo, na pia ulinzi ulikuwa wa hali ya juu, takribani polisi 450 walikuwepo.

Wanawake walishauriwa kuja na mavazi zaidi ya matatu ili kuzuia nguo kugongana/kufanana.

Zaidi ya marafiki 250 na familia-wakiwamo wachezaji wakubwa mbalimbali walikwea pipa mpaka Argentina kuhudhuria harusi ya nyota huyo.

Samuel Eto'o alikuja na mkewe Georgette, Aguero na mpenzi wake Karina, Fabregas alikuwa na mchumba wake Daniella Seaman, rafiki wa Antonella na mchezaji wa timu ya Taifa ya Argentina Ezequiel Lavezzi nae alikuwepo, Neymar, Pique na mke wake Shakira, Puyol,Jordi Alba, Xavi,Sergio Busquets, Luis Suarez na wengine wengi walikuwepo na wake/wapenzi wao katika harusi hiyo.

Leo Messi,30, na Antonella Roccuzzo,29 tayari wana watoto wawili wa kiume, Thiago na Mateo.


Baadhi Ya Picha Za mastaa Mbali Mbali Wa Soka Waliohudhuria Sherehe Hiyo

No comments

Powered by Blogger.