Header Ads

Mchezaji wa klabu ya RB Leipzig na timu ya taifa ya Denmark Mwenye Asili Ya Tanzania Atua Tanga Kwa Ndugu Zake


Mchezaji wa klabu ya RB Leipzig na timu ya taifa ya Denmark, Yussuf Poulsen amewasili Tanga nchini Tanzania ambapo ndio asili ya baba yake.
Mchezaji wa kimataifa wa Denmark na klabu ya RB Leipzig inayoshiriki ligi ya Ujerumani (Bundesliga),Yussuf Poulsen (kulia)
Poulsen raia wa Denmark, ambapo ndipo kwenye asili ya mama yake, lakini baba yake ambaye alishafariki, ni mdigo wa Tanga, ni mchezaji anayekipiga kwenye timu inayoshiriki Ligi kuu ya nchini Ujerumani (Bundesliga) RB Leipzig.
Baba wa mchezaji huyo alifariki kutokana na maradhi ya kansa wakati Poulsen akiwa na umri wa miaka sita, kwa sasa Yussuf Poulsen yupo jijini Tanga, kutembelea familia ya upande wa baba yake.

No comments

Powered by Blogger.