Header Ads

THE SAGA CONTINUES: barakah asema mziki wake ulidrop rockstar4000

Baada ya taarifa za kujitoa kweny label iliyokuwa inasimamia muziki wake, pamoja  na baadhi ya mashabiki wake kumlaum kwa kujitoa  huko Barakah the prince leo katoa sababu za kutoka kwake rockstar4000

Baraka da prince amedai kuwa muziki wake ulishuka kiwango mara baada ya kusaini mkataba na label ya 'RockStar4000' kitu ambacho ni tofauti na mategemeo yake .

Mkali huyo wa 'Acha Niende' ambae hivi sasa ameenda kufanya kazi na label yake binafsi 'Bana Music Entertainment' amesema kuwa maoni hayo kuhusu muziki wake kushuka alikuwa akiyapata kwa mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa Instagram .

. . "Mashabiki zangu wamekuwa wakilalamika sana kwenye page yangu Barakah imekuwaje mbona utaratibu wako wa kazi sio kama zamani sio kama ulivyokuwa ukifanya kazi na watu wengine kwahiyo mwisho wa siku hata watu wa nje hata mashabiki pia wanaliona hilo kwamba utendaji wa kazi wa Barakah ume'drop everything imeenda tofauti na ambavyo mimi nilitegemea" alifunguka DA Prince

Kuhusu kufanya kazi na management nyingine baada kutoka RockStar Barakah amesema "sipo tayari kuwa chini ya mtu yeyote kwa kipindi hichi otherwise kuwe kuna makubaliano ya nguvu sana sijui yani kutakuwa na makubaliano gani"

No comments

Powered by Blogger.