Header Ads

Taifa Stars Kibaruani Tena Kukipiga Na Zambia

Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) leo inanaingia uwanjani kumenyana na timu ya taifa ya Zambia ‘Chipolopolo’ katika hatua ya Nusu Fainali ya michuano ya COSAFA Castle mchezo utakao pigwa katika dimba la Moruleng wenye uwezo wa kuingiza watu 20,000, uliopo nje kidogo ya mkoa wa Rustenburg.
Rustenburg ni miji yenye baridi kali nchini Afrika Kusini ukijijenga chini ya safu za milima ya Magaliasberg katika jimbo la kaskazini magharibi.
Jotoridi hushuka mpaka nyuzi 5 lakini kwa sasa imesimamia 11 ni tofauti kubwa na jiji la Dar es salaam ambalo huchezea 28 mpaka 32!.
Huu ni mtihani mwingine wa hali ya hewa kwa timu yetu ya Tanzania.
Zambia (Chipolopolo) imefika Nusu Fainali baada ya kuitoa Botswana kwa kuifunga 2-1 Jumamosi, wakati Tanzania iliwatoa wenyeji Afrika Kusini kwa kuwachapa 1-0.
Mchezo wa nusu fainali kati ya Zambia na Taifa Stars umekuwa gumzo katika michuano hiyo kutokana na mafanikio ya Stars mpaka sasa kama timu waalikwa.
Mara ya mwisho Zambia na Tanzania kukutana katika michuano hiyo ni Julai 5 , 1997 jijini Arusha katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid na ‘ Chipolopolo ‘ ikienda sare ya 2-2 na Taifa Stars.
Na Julia 5, 2017 Tanzania itakutana tena na Zambia katika michuano ya Cosafa huku Stars ambayo imecheza mechi 4 mfululizo bila kupoteza na kuweka rekodi ya kutoa Man of da Match kila mchezo ikisubiri kurra za Mungu iliiweze kupita katika miamba ya Chipolopolo ambayo inaonekana kupigiwa upatu wa kutinga hatua ya fainali
Kwa ujumla, kabla ya leo, timu hizo zimekwishakutana mara 30, Tanzania ikishinda mechi tano na Zambia ikishinda mechi 16, huku mechi tisa zikiisha kwa sare. Julai 5 kama leo, mwaka 1997 zilikutana katika Kombe la COSAFA pia na na zikamalizana kwa sare ya 2-2, lakini leo lazima mshindi apatikane.
Tanzania ilianzia hatua ya mchujo kwenye Kundi A ambako iliongoza kwa pointi zake tano sawa na Angola baada ya sare mbili 0-0 na Angola, 1-1 na Mauritius na ushindi wa 2-0 dhidi ya Malawi, hivyo kutengeneza wastani mzuri wa mabao na kuwapiku wapinzani kusonga Nusu Fainali.
Zambia yenyewe ilianzia moja kwa moja hatua ya Robo Fainali sawa na Afrika Kusini, Botswana,
Namibia, Lesotho na Swaziland huku Zimbabwe ikiongoza Kundi B. Lesotho na Zimbabwe zitamenyana katika Nusu Fainali ya pili Saa 2:00 usiku.
Beki Abdi Hassan Banda anatarajiwa kurejea kwenye kikosi cha kwanza cha Taifa Stars leo baada ya kumaliza kutumikia adhabu ya kadi, lakini kocha Salum Mayanga anaweza kuwakosa majeruhi beki Shomary Kapombe na kiungo Raphael Daudi walioumia kwenye mchezo wa Nusu Fainali dhidi ya Afrika Kusini.

No comments

Powered by Blogger.