Header Ads

Alichojibu Izzo Bizness Baada Ya Kuulizwa Kuhusu Collabo Za Kimataifa

Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Izzo Bizness amedai kwa sasa bado ni mapema kufanya kolabo na wasanii wa nje.
Image result for izzo bizness
Rapper huyo ambaye ameachia wimbo mpya ‘Rafiki’, amesema ingawa kuna baadhi ya wasanii wamekuwa katika mazungumzo ya mara kwa mara ila bado anaangalia iwapo wakifanya kazi pamoja matokeo yake yatakuwa ni yapi.
“Hiyo ni mipango tu kwa sababu hata Khaligraph, Navio, washikaji wa Camp Mulla, Avril watu wengi wakina King Kaka nipo naongea nao, na uzuri tushakuwa na connection,” Izzo Bizness alizungumza kupitia Planet Bongo ya EA Radio na kuongeza.
“Kwa hiyo ni mipango tu, unajua siku zote biashara yako inakuwa unaipeleka kwa mipango, si vitu ambavyo unavifanya kwa sifa uje hapa useme nilifanya na fulani, impact yake ni nini. Kwa hiyo vitu vyote vitanyika tunahitaji muda tu,” alisistiza Izzo.

No comments

Powered by Blogger.