Header Ads

Jua Cali - Ray Vanny Kainyanyua Afrika Mashariki

Siku Kadhaa Baada Ya Rayvanny Kuibuka Mshindi wa tuzo ya BET International Viewers Choice, Rapa Mkongwe kutoka Kenya, Jua Cali Amempongeza Baada Ya Kuguswa Na Ushindi Huo.
Image result for rayvanny bet awards 2017
Akitiririka, Jua Cali, aliyeivaa jarida la Parents toleo la hivi majuzi pamoja na mkewe wa miaka minane, amemsifia msani huyo kutoka WCB, kwa kusema ushindi wake unaupa sifa muziki wa East Afrika kwa kuutangaza zaidi.
Unajua ndoto yetu sisi wote ni kupeleka ngoma za East Afrika huko nje. Unajua Ushindani Ni Mkubwa Sana, tunapigana na watu wa South Africa, West Africa, Marekani, watu wa Europe. Ikitokea msanii wetu anashinda tuzo kama hiyo, ni kitu kikubwa .
Image result for juacali
Kwa sababu sasa kinaweka East Afrika mahali pazuri hasa ukizingatia muziki wetu tunaimba  kiswahili. Aliendelea Kusema "Unajua mimi ni mtu wa Kiswahili so nikiona msanii anaimba kwa Kiswahili na ameshinda inapendeza sana.”
Kuhusu ujio wake mpya, Juacali ambaye mapema mwaka juzi alitangaza kwamba atapunguza kasi za muziki ili kujishughulisha zaidi na utengenezaji Wa Muziki, kaahidi kuachia albamu yake ya nne Septemba mwaka huu aliyoiita ‘Mali ya Umma’.

No comments

Powered by Blogger.