Header Ads

Manny Pacquiao Achakazwa Na Mwalimu Wa Shule Ya Msingi Huko Australia

Jeff Horn and Manny Pacquiao
Mwalimu wa zamani wa shule ya Msingi nchini Australia Jeff Horn ameshangaza ulimwengu wa ndondi kwa kumshinda bingwa wa dunia raia wa Ufilipino Manny Pacquiao

Jeff Horn alishinda kwa pointi katika pambano la raundi kumi na mbili na kupata taji la welterweight mbele ya mashabiki elfu hamsini (50,000)  lililofanyika kwenye Uwanja wa Suncorp huko Brisbane, Australia

Kabla ya pambano hilo kuanza watazamaji wengi walidhani kuwa Horn mwenye umri wa miaka ishirini na tisa (29)  hakuwa na nafasi yoyote ya kushinda mbele Manny Pacquiao.

Jeff Horn,29 ,ambaye ni mwalimu wa zamani wa  shule ya msingi Pallara State  amebuka mshindi dhidi ya Pacquiao,38 baada ya majaji kumpa ushindi wa pointi 117-111, 115-113 na 115-113.
Jeff Horn celebrates winning the world title


 Kushindwa kwa Manny Pacquiao kumewashangaza mashabiki wengi nchini ufilipino Na Duniani Kwa Ujumla
Pacquiao ambaye ana umri wa thelathini na nane ni mmojawapo wa wanamasumbwi mashuhuri wa kizazi cha sasa

No comments

Powered by Blogger.