Header Ads

Young Killer Msodoki Amchana Tena Nay Wa Mitego

Image result for young killer msodoki
Msanii wa muziki wa hip hop Young Killer Msodoki amedai kama Nay wa Mitego anataka yeye arudi kwa bosi wake wa zamani Mona Gangsta, basi na rapa huyo kurudi kwa producer wake wa zamani Mr T-touch huku akidai Nay hajawahi kutengeneza ngoma kali toka aachane na producer huyo.
Wawili hao wameingia kwenye mgogoro wa kurushiana maneno baada ya rapa Nay wa Mitego kumchana Young Killer kwamba amefulia na baadaye Young Killer kujibu kupitia wimbo wake wa True Boya.
Rapa Young Killer amedai Nay wa Mitego hakufanya utafiti wowote kabla ya kuachia wimbo wake huo ambao ndani yake amewachana wasanii wengi.
“Nay anasema nirudi kwa Mona, kama kweli anataka mimi nirudi kwa Mona angeanza kwanza yeye kurudi kwa T-touch kwa sababu toka aachane naye hajatoa ngoma yoyote kali,” Young Killer alikimbia kipindi cha FNL cha EATV.
Image result for young killer msodoki true boya
Aliongeza, “Tatizo la Nay anazungumza vitu bila kufanya utafiti, mimi kama nataka kufanya kitu lazima nifanye utafiti kwanza sio yeye anakuruputa na kuzungumza vitu ambavyo havina hata msingi,”
Rapa huyo amedai wimbo ‘True Boya’ sio rasmi kwani anajipanga kuachia kazi zake mpya pamoja na kolabo zake.

No comments

Powered by Blogger.