Header Ads

Haya hapa maneno ya aslay kuhusu kujiunga WCB

Baada ya kuenea kwa tetesi za msanii wa yamoto band, Maromboso kuwa yupo mbioni kusainiwa WCB. Member mwingine wa kundi hilo Aslay ameibuka na kudai kuwa yeye hawezi kusaini WCB wala ROCKSTAR4000 .
Aslay amesema kuwa ndoto yake ni kuwa mkubwa zaidi ya WCB na sio kusainiwa na lebal hiyo au nyingine yeyote .
"Kusainiwa WCB..? Aah hapana! Kwasababu mimi nina ndoto ya kuwa zaidi ya WCB au kuwa zaidi ya kitu kingine chochote kwahiyo nitakaza na mimi naamini nitafika zile sehemu kwasababu nina ndoto ya kufika level aliyofika Chibu, nina ndoto ya kufika alipofika Alikiba kwahiyo inabidi nikaze mimi kama mimi nitafute njia ya kutoboa nifike level zile, kwa label yeyote ile wakisema wanisaini siwezi kukubali" alisema asley

No comments

Powered by Blogger.