Header Ads

Barnaba kayasema haya kuhusu wasanii wenzake wa bongo fleva

Mwimbaji hodari na mtunzi wa muziki wa bongo flavour kutoka  Tanzania, BARNABA, amezungumza kinaga ubaga kinachousibu muziki wetu, na kushindwa kupiga hatua.

Akizungumza na Mtangazaji Jr. Junior wa EA RADIO, kwenye kipindi cha Bongo Fleva Top 20, Barnaba  alisema, wasanii wenyewe ndio wanaushusha muziki kwa dhana zao za kufunikana,

"Kinachoua muziki wetu ni Ushindani wa wenyewe kwa wenyewe na kushindwa kupeana nafasi. Ndio maana tunashindwa na wenzetu wa Nigeria na Kwingineko" alisema Barnaba

"Unakuta mtu anafanya wimbo ili amfunike mwezake, tena sasa hivi limezuka hili la kupandiana kwa juu, yaani mtu anarekodi ngoma zake na video anaziweka ndani, akisikia Barnaba katoa wimbo na yeye anapandia kwa juu kwa lengo la kufunikana." alimaliza Barnaba

BARNABA BOY CLASSIC ambaye  kwa sasa anasumbua masikio yetu kwa dude lake jipya, TUNAFANANA. Ni msanii mkongwe na mwandishi nguli kabisa wa nyimbo za bongo flavour akiwa kawaandikia wanamuziki wengi akiwamo vanessa mdee Nandy na Shilole.

No comments

Powered by Blogger.