Tetesi Za Usajili Barani Ulaya
Manchester City sasa wanaongoza katika mbio za kumsajili Alexis Sanchez, 28, baada ya Bayern Munich kujitoa kutokana na bei kubwa ya mchezaji huyo wa Arsenal (Daily Mirror).
Manchester City wana uhakika wa kumsajili Alexis Sanchez kwa takriban pauni milioni 50, kwa sababu mchezaji huyo anatamani kufundishwa na Pep Guardiola (Guardian)
Chelsea wanakabiliwa na ushindani kutoka Paris St-Germain katika kumsajili beki Alex Sandro, 26, huku Juventus wakitaka pauni milioni 61 (Daily Mail).
Chelsea wanatazamiwa kukamilisha usajili rasmi wa Tiemoue Bakayoko kutoka Monaco wiki hii (The Sun).
Wakala wa kiungo wa Chelsea Mario Pasalic, wamekutana na Real Betis kujadili uhamisho wa mchezaji huyo kwenda Spain (Marca).
Manchester United watazidiwa kete na Paris St-Germain katika kumsajili kiungo kutoka Brazil, Fabinho, 23 anayechezea Monaco (Daily Record).
Dau la Arsenal la zaidi ya pauni milioni 30, la kumtaka winga wa Monaco, Thomas Lemar, 21, limekataliwa, na sasa Arsenal wanafikiria kukamilisha usajili wa Riyad Mahrez, 26, kutoka Leicester (Telegraph).
Barcelona, Manchester City na Chelsea ni miongoni mwa timu zinazomnyatia winga wa Monaco, Thomas Leimar (L"Equipe).
Arsenal wanamtaka kiungo wa Nice Jean Michael Seri, 25, baada ya Roma kukatishwa tama na bei ya pauni milioni 35 kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast (The Sun)
Mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud anakaribia kurejea Ufaransa, huku Lyon na Marseille wakimtaka, na Arsenal ikitafuta mtu wa kuziba pengo lake (L'Equipe).
Chelsea huenda wakatibua dau la Zenith St Petersburg la pauni milioni 26 la kumtaka beki wa Roma, Kostas Minolas, huku mchezaji huyo pia akisita kuhamia Urusi (Daily Telegraph).
Michel Keane hatarajiwi kurejea Burnley kwa sababu Everton wanatarajiwa 'kulazimisha' usajili wake kabla ya kumalizika kwa wiki hii (Burnley Express).
Michael Keane atagharimu pauni milioni 25 (Times).
Mshambuliaji wa Watford Stefano Okaka, 27, amepewa dau kubwa la kuhamia Shanghai Shenhua ya China (The Sun).
Arsenal wameambiwa lazima walipe pauni milioni 57 ili kumsajili Alexandre Lacazette, 26, kutoka Lyon (London Evening Standard).
Kinda wa Arsenal Kaylen Hinds anajiandaa kuondoka Emirates na kujiunga na Wolfsburg ya Ujerumani (The Sun).
Mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale yuko tayari kuondoka Spain na kuhamia Manchester United (Daily Star).
AC Milan wanapanga kutoa kitita kikubwa kumsajili kiungo wa Real Madrid Isco (Don Balon).
AC Milan wanakaribia kumsajili Hakan Calhanoglu kutoka Bayer Leverkusen kwa euro milioni 20 (Sky Sport Italia).
West Brom wanakaribikia kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Southampton Jay Rodriguez, 27 kwa pauni milioni 12 (Daily Express).
Nahodha wa zamani wa Chelsea John Terry, 36, ameambiwa anaweza kuchukua nafasi ya umeneja wa Aston Villa, iwapo atajiunga na klabu hiyo (Daily Express).
Mchezaji anayenyatiwa na Liverpool Naby Keita, 22, amesema angependa kuchezea moja ya timu kubwa kama vile Barcelona, Real Madrid au Manchester City. Liverpool wanamtaka kiungo huyo wa Red Bull Leipzig (Manchester Evening News).
Beki wa Chelsea Nathan Ake, 22, anakaribia kufanikisha uhamisho wake wa pauni milioni 20 kwenda Bournmouth (Guardian).
Pierre Emerick-Aubameyang, 28, anawaniwawa na Liverpool anaonekana kukaribia kukamilisha uhamisho wake kwenda Tianjin Quanjian ya China, ambayo imetoa dau la pauni milioni 70 (Daily Star).
Real Madrid bado wanafikiria kuhusu Kylian Mbappe, kwa mujibu wa Rais wa Real, Florentini Perez, ambaye anasema umri wake wa miaka 18 huenda ukawa tatizo katika klabu hiyo ingawa amekiri kuwa Zinedine Zidane yuko karibu na mchezaji huyo na usajili unaweza kufanyika (Independent).
Winga wa Everton Gerard Deulofeu, 23, amekataa nafasi ya kurejea Barcelona, huku AC Milan na Juventus pia zikimtaka (Daily Mail).
Newcastle United wanazungumza na Liverpool kuhusu uhamisho wa mkopo wa winga Sheyi Ojo, 20 (Newcastle Chronicle).
Mkurugenzi mkuu wa Southampton Les Reed amesisitiza kuwa mabeki wake Virgil van Dijk na Cedric Soares hawauzwi. Liverpool na Tottenham zinawataka wachezaji wao (Sky Sports).
Leicester City hawajapokea dau lolote la kumtaka Riyad Mahrez, ambaye amehusishwa na kuhamia Arsenal, Barcelona na Chelsea (Leicester Mercury).
Juventus wanafikiria kumchukua beki wa Real Madrid Danilo, kuziba nafasi ya Dani Alves anayetazamiwa kwenda Manchester City (Corriere dello Sport).
Manchester City Wanahitaji Kumsajili Winga Wa Bayern Munich Kingsley Coman (RMC)
Barcelona Wanawatazama Ander Herrera na Riyard Mahrez Kama Mbadala Iwapo watashindwa Kumsajili Marco Verratti (Sport.es)
Barcelona Wanawatazama Ander Herrera na Riyard Mahrez Kama Mbadala Iwapo watashindwa Kumsajili Marco Verratti (Sport.es)
No comments