Header Ads

Ronaldo Athibitisha Kupata Mapacha Wa Kiume

Mchezaji bora wa dunia anayechezea timu ya taifa ya Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amethibitisha rasmi kwamba amekuwa baba wa watoto wengine wawili wa kiume ambao ni mapacha.
Cristiano Ronaldo to leave Portugal squad to be with newborn sons
Ronaldo ambaye amekuwa akihusishwa kuhamia Manchester United baada ya kuingia katika tuhuma za ukwepaji kodi nchini Hispania, amethibitisha ujio wa watoto hao mapacha mara baada ya timu yake ya taifa ya Ureno kutolewa katika michuano ya mabara inayoendelea nchini Urusi.

Ronaldo alibaki Mwenye Huzuni Baada Ya Timu Yake Kuondolewa Kwenye Mashindano, Ila Hakusita Kuujuza Ulimwengu Kupitia Mtandao Wa Facebook Ambapo Aliandika Kwamba "Nilikuwa Naitumikia Timu Yangu Ya Taifa Kimwili Na Kiroho Ijapokuwa Watoto Wangu Wawili Wa Kiume Walikuwa Wamezaliwa Bahati Mbaya Hatujaweza Kufikia Lengo Letu Kuu Ila Naamini Tutaendelea Kuwa Tumaini La Wareno Siku Zijazo, Rais Wa Chama Cha Soka Cha Ureno Na Timu Ya Taifa Wamenionesha Mwenendo Ambao Umenigusa Na Sitosahau Nafurahi Sana Kuwa Na Watoto Wangu Kwa Mara Ya Kwanza"
Image result for ronaldo georgina and cristiano jr
Ujio wa watoto hao wawili unamfanya mchezaji huyo kuwa na jumla ya watoto watatu kwakuwa tayari alishakuwa na mtoto mmoja wa kiume Aliyefikisha Umri Wa Miaka Saba Mapema Mwezi Huu.

No comments

Powered by Blogger.