Header Ads

Roma - Moto Wangu Kwenye Show Haujapungua, Sana Sana Umeongezeka

Msanii wa Bongo Fleva, Ibrahim Musa Maarufu Kama Roma amesema kwa sasa yupo kamili Gado katika kufanya show

Kauli ya Rapper huyo inakuja baada ya kuugulia kipindi kirefu cha maumivu tangu alipopatwa na mkasa wa kutekwa. Hapo juzi Roma alifanya show kwa mara ya kwanza.
“Uwezo wangu kwenye performance nipo poa, am good enough, strong enough, hakuna chochote ambacho kimebadilika sana sana kimezidi tu kwa sababu nilikuwa nayaona mapokezi ya watu kabla sijafanya show,” alisema hayo kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM na kuongeza.
“Hii ndio carrier yangu, ni kama kujua mpira ukijua umejua tu, kwa hiyo technique zile za ku-perform ambazo ninazo zinabakia pale pale, Roma waliyemuona 2005, 2014 nadhani ndio huyo huyo,” amesema Roma

No comments

Powered by Blogger.