Header Ads

CRISTIANO RONALDO AENDELEA KUWA MWIBA KWA TIMU PINZANI LIGI YA MABINGWA ULAYA

Usiku Wa Jana Ulikuwa Ni Usiku Wa Mwendelezo Wa Ubabe Wa Mchezaji Bora Wa Dunia Kwa Sasa Cristiano Ronaldo Baada Ya Kuwatungua Atletico Madrid Goli Tatu
Sherehe Ya Magoli Ya Cristiano Ronaldo Ilianza Mapema Dakika Ya 10 Baada Ya Pasi Safi Kutoka Kwa Casemiro Na Hivyo Kufanya Matokeo Kuwa Real Madrid 1-0 Atletico Madrid Mpaka Half Time
Kipindi Cha Pili Kilianza Kwa Kasi Ndogo Lakini Real Madrid Walianza Kuimarika Kila Muda Ulipokuwa Unasogea Mpaka Kufikia Dakika Ya 73 Ronaldo Akarudi Tena Kambani Baada Ya Pasi Maridadi Kutoka Kwa Benzema
Hiyo Haikufanya Real Madrid Waache Kutafuta Magoli Zaidi Dakika Ya 86 Lucas Vazquez Alifanya Movement Nzuri Iliyo Zaa Goli La Tatu Lililofungwa Na Cristiano Ronaldo Kwa Mara Nyingine Tena Hivyo Kufikisha Idadi Ya Magoli 10 Ya Ligi Ya Mabingwa Ulaya Msimu Huu Ikiwa Ni Magoli 8 Katika Mechi 3 Zilizopita Goli 5 Dhidi Ya Bayern Munich Na Goli 3 Dhidi Ya Atletico Madrid
Hat trick Ya Jana Imemfanya Cristiano Ronaldo Kuwa Mchezaji Wa Kwanza Kufunga Hat trick Mara Mbili Mfululizo Katika Hatua Ya Mtoano Pia Ronaldo Kafikisha Goli 50 Kwenye Hatua Ya Mtoano Ligi Ya Mabingwa Na Kumfanya Awe Mchezaji Wa Kwanza Pia Kufikisha Idadi Hiyo Ya Magoli
Champions League - Semi-finals May 2
FT Real Madrid 3 - 0 Atletico Madrid
10' Cristiano Ronaldo 1 - 0
73' Cristiano Ronaldo 2 - 0
86' Cristiano Ronaldo 3 - 0
1st leg, aggregate score:(3 - 0)

No comments

Powered by Blogger.