Header Ads

BURUDANI: CHRIS BROWN KAWEKA HISTORIA NYINGINE

Msanii nguli wa miondoko ya RnB kutoka nchini marekani,Christopher Brown alimaarufu Chirs Brown ameweka rekodi mpya katika mtandao wa you tube kwa kupata subscribers million kumi (10m) hivo kutunukiwa diamond button
Brown anaungana na mastaa wengine kama Rihanna, Eminem, Skrillex,  Taylor swift, Nick minaj, Wiz Khalifa na ariana grande  wote wakiwa na diamond buttons
Ni youtuber mmoja mpaka sasa, Pewdiepie mwenye ruby button kwa kuwa na subscribers million 55.
Chris Brown alionesha furaha yake kwa kupost barua aliopokea kutoka youtube katika mtandao wa instagram akisindikiza na caption "thank you youtube"
Utaratibu wa kutambua channel za youtube zenye subscriber wengi umeanza hivi karibuni ambapo channel zinazovuka subscribers laki moja wanapata silver button, channel zenye subscribers zaid ya million moja wanapata gold button na zinazovuka subscribers millioni kumi  wanapata diamond button. Ruby button aliyopata pewdiepie haipo kwenye orodha ya buttons zinazotolewa na youtube na haijulikani utaratibu gani ulitumika kumpatia button hiyo na kama mtu mwingine akipata subscribers hao haijulikani kama atapewa nae ruby button ama la.
Ikumbukwe pia utaratibu huu upo tofauti na hauingiliani na youtube awards, tuzo zinazotolewa na youtube kutambua video zenye ubora zaidi

No comments

Powered by Blogger.