Header Ads

Biashara asubuhi jioni mahesabu, Real Madrid mabingwa wa ndani na nje ya mchezo

Fainali ya Uefa mbele yao, Hatima ya La Liga mikononi mwao, Mabingwa wa Kihistoria nchini Uhispania klabu ya Real Madrid inaelekea kumaliza msimu huu vizuri, Mabingwa hao wa Dunia hivi Leo wanashuka dimbani kumalizia mchezo wao wa Kiporo dhidi ya Celta Vigo.
Licha ya ukweli kuwa Celta wanawasumbua sana Real Madrid bado morali ya kutwaa ubingwa huo haitashuka, ikiwa takribani miaka mitano kombe hilo hawajalichukua, endapo wakishinda Leo Real watakua wamejihakikishia ubingwa kwa asilimia 99 huku wakingoja angalau wasuluhu tu katika mechi yao ya mwisho dhidi ya Malaga.

Hakuna namna Malaga ashinde dhidi ya Real Madrid, kwanini ? Kwasababu Madrid watakua hawana cha kupoteza ndani ya dimba la Santiago bernabeu , vile vile Club ya Malaga itapata mgao wa uhamisho wa isco endapo Vigogo hao watatwaa ubingwa ukizingatia Malaga hawana cha kugombania msimu huu wanatazimiwa kucheza mechi hiyo kwa ajili ya kukamilisha ratiba tu.

Nje ya uwanja Real hawana wasiwasi na mauzo ya jezi, wana mikataba lukuki kutoka fly emirates, hospital ya sanitas , makampuni ya ujenzi ya Perez pamoja na masuala mengine mengi ikiwemo mikataba ya wachezaji ambazo Real huchukua asilimia kadhaa, vile vile mauzo ya matangazo , matangazo ya television, hotel zao, maduka nje ya uwanja wao wa mazoezi pamoja na hazina kibao jijini humo.

Kila mchezaji aliyeko real ni ghali, hakuna namna unaweza ukamchukua kirahisi labda kama hawana cha kuongeza kwake, wameweka thamani katika kila mchezaji, mfano Liverpool walivyojaribu kumnasa kinda wao aliyejuu  kwasasa Marcus Asensio walitajiwa paund Million 54 , hawakurudi tena lakin ndivyo walivyo Madrid yaani kuanzia first eleven hadi wakalia benchi hawashikiki kirahisi sokoni,

Licha ya kiungo maridadi James Rodriguez kucheza mechi chache mwanzoni mwa msimu kutokana na ushindani katika eneo la kiungo, bado ni Biashara nzuri sokoni kupita zote, kwanini? Statistics zinambeba sana James kiasi kwamba lazima wanunuzi washawishike, amefunga magoli mengi na kusaidia kutengeneza kila akipopata nafasi, vile vile James ni mmoja kati ya wachezaji wenye mvuto dunuani kwahiyo ameuza jezi za kutosha sana, na tayari rafiki yake ambae ni Mchezaji bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo, ameshamshawishi mkolombia huyu kwenda Old Trafford, muda utaongea, na tayari bei yake ya Maulizo ni euro 42m.

Hao ndo mabingwa wa kamari, mabingwa wa Dunia, Real Madrid

No comments

Powered by Blogger.