HAWA NDIO MASTAA 7 WANAONGOZA KWA MITUNGO BONGO
BAADHI ya mastaa Bongo wamekuwa na tabia ya kubadilisha
wanaume baada ya muda mfupi wanapokuwa nao kwenye uhusiano wa kimapenzi kitu
ambacho kinaleta picha tofauti kwenye jamii ambayo wanawaangalia wao kama kioo
cha jamii na kuwafanya waonekane kama watu ambao hawana mafunzo yoyote.
Kipindi hiki imekuwa kama fasheni kwa baadhi ya mastaa
kuchuana live kwa mitungo ya ngono, yaani wanaanika uhusiano na mpenzi huyu
jamii yote inajua kisha baada ya kipindi f’lan wanatemana na kuanzisha na
mwingine.
Katika makala hii, nachambua mastaa saba ambao wanachuana
live kwa mitungo ya ngono;
Wastara.
WASTARA
Unaweza kusema naye ana bahati mbaya katika mlolongo mzima
wa kimapenzi tangu afariki mumewe, Juma Kilowoko ‘Sajuki’. Mara nyingi
anapoingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na mtu anaishia kuumizwa kitu ambacho
kinamfanya kutodumu na mpenzi mmoja.
Ikumbukwe kuwa, baada ya Sajuki kufariki aliingia kwenye
mapenzi na msanii mwenzake, Bond Suleiman ambaye naye hawakudumu muda mrefu
wakaachana na hatimaye aliolewa na Mbunge wa Donge, Sadifa Juma.
Kwa mbunge huyo napo hakudumu, alikaa naye kwa muda mfupi
kisha wakaachana na kumrudia Bond.
Juzikati alitemana na Bond kila mmoja akimtupia maneno
mazito mwenzake lakini kwa sasa ameamua kuupoza moyo wake kwa kuingia katika
penzi jipya na ‘serengeti boy’ aliyefahamika kwa jina la Jukya.
Nisha.
NISHA
Salma Jabu ‘Nisha’ ni mmoja wa waigizaji wazuri wa
vichekesho na maigizo lakini na yeye hakuwahi kuwa na mlolongo mzuri wa wanaume
aliotoka nao kimapenzi.
Alianza kuanika uhusiano na msanii wa Bongo Fleva, Emmanuel
Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ambapo uhusiano wao haukudumu. Alikaa kimya kwa muda
akaibuka na msanii mwingine, Barakah The Prince ambaye naye hakudumu muda mrefu
na sasa yupo katika penzi jipya na ‘serengeti boy’ anayejulikana kwa jina moja
la Minu.
Wolper.
JACQUELINE WOLPER
Ni mmoja kati ya mastaa ‘grade one’ kwenye filamu Bongo,
kama ilivyo kwa Wastara na Nisha, uhusiano wake wa kimapenzi umekuwa hauna
mzani uliotulia kwa kuwa mara nyingi amekuwa akibadilisha wanaume muda mfupi tu
anapokuwa ameingia nao kwenye uhusiano wa kimapenzi.
Nyuma kidogo staa huyo ambaye ana msururu mkubwa wa wanaume
waliompitia alikuwa penzini na msanii wa Bongo Fleva, Harmonize lakini
hawakudumu muda mrefu waliachana na kugeukia penzi jipya la kijana
anayefahamika kwa jina moja la Brown.
Uwoya.
UWOYA
Anaingia kwenye orodha ya mastaa wenye mtungo wa kimapenzi
baada ya kusikika kwa skendo zake mbalimbali za kimapenzi tangu alipoachana na
mumewe, Hamad Ndikumana.
Baada ya kutemana na mumewe, alisikika kutoka kimapenzi na
mwanamuziki Linex kisha Msami Baby, Quick Racka na juzikati alihusishwa kutoka
kimapenzi na mwanamuziki Dogo Janja.
Kajala.
KAJALA
Kama ilivyo kwa mastaa wengine hapo juu, Kajala naye ni
miongoni mwa mastaa wanaoongoza listi ya kuchuana kwa kuwa na msururu mrefu wa
wanaume.
Alishawahi kuwa na uhusiano na Petit Man, CK na baadaye
msanii wa Bongo Fleva, Quick Racka.
Shilole.
SHILOLE
Ni miongoni mwa mastaa waliopo kwenye listi ya kuwa na
uhusiano na wanaume tofautitofauti ndani ya kipindi kifupi
Ikumbukwe kuwa alianza uhusiano na msanii wa Bongo Fleva,
Barnaba kisha Nedy Music ambaye hakudumu naye na kuingia katika penzi na Nuh
Mziwanda.
Hata hivyo hakudumu na Nuh, akaingia katika penzi jipya na
msanii mwingine, Hamadai kisha akaenda Mr Kesho kabla ya hivi karibuni kuhamia
kwa mwanaume anayefahamika kwa jina la Uchebe.
Wema.
WEMA
Naye anaibeba listi ya mastaa ambao hawadumu katika mapenzi,
mrembo huyu alianza kuhusishwa kuwa katika uhusiano na wasanii Mr. Blue na TID
kabla ya kuingia kwa marehemu Kanumba.
Hakudumu na Kanumba akaingia kwa mjasiriamali, Jumbe Yusuf
ambaye alitangaza hadi ndoa iliyokuja kuyeyuka ghafla. Baada ya Jumbe, Wema
alizama kwa msanii wa Dansi, Chaz Baba ambaye naye hakudumu na kuzama kwa
msanii wa Bongo Fleva.
Haikuishia hapo, aliingia kwa mshiriki wa Big Brother Africa
‘Hotshots’ 2014, Luis Mnana ambaye ni raia wa Namibia ambapo hawakudumu na
kuingia kwa Idris.
SOURCE: GLOBAL PUBLISHERS
No comments