Tetesi Za Usajili Barani Ulaya
wa Chelsea Diego Costa, 28, yuko tayari kuwa na mazungumzo na Antonio Conte, na huenda akaichezea tena klabu hiyo msimu ujao. Costa alitumiwa ujumbe mfupi wa simu (SMS) na Conte kuambiwa kuwa hahitajiki tena Stamford Bridge (Sun).
Chelsea wanataka zaidi ya pauni milioni 60 kumuuza Diego Costa, na watamuuza hata ikiwa Romelu Lukaku ataamua kujiunga na Manchester United (Daily Mail).
Huku Romelu Lukaku akikaribia kujiunga na Manchester United, Chelsea sasa huenda wakaelekeza nguvu zao kumtaka Andrea Belotti, 23, kutoka Torino na watalazimika kulipa takriban pauni milioni 90 (Daily Mirror).
Mkataba wa Romelu Lukaku kutoka Everton kwenda Manchester United ni pauni milioni 75 za awali na ada hiyo itapanda hadi pauni milioni 90 (Sky)
Antonio Conte sasa anataka kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Man Utd Javier "Chicharito" Hernandez kwa pauni milioni 13.5 baada ya dau lao la dakika za mwisho kutaka kumsajili Lukaku kushindikana (The Sun).
Wayne Rooney anajiandaa kukata mshahara wake kwa nusu hadi pauni 150,000 kwa wiki kujiunga na Everton kutoka Manchester United (Daily Mail).
Wayne Rooney amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili kwenda Everton kutoka Manchester United (Daily Star).
Manchester United wataelekeza nguvu zao kumtaka kiungo wa Tottenham Eric Dier, 23, kwa pauni milioni 50 mara watakapokamilisha mkataba wa Lukaku (Telegraph).
Manchester United wameongeza bidii katika mazungumzo ya kutaka kumsajili kiungo wa Real Madrid James Rodriguez (The Independent).
Manchester United watalazimika kusubiri hadi mwezi Januari kupanda dau kumtaka beki wa kulia wa Benfica Nelson Semedo (Correio da Manha).
Arsenal wanasubiri jibu kutoka Monaco kuhusu kupanda dau la pauni milioni 40 kumtaka winga Thomas Lemar, 21 (Football London).
Arsenal wanamtaka kipa wa Toulouse Alban Lafont, 18, ili kuwa mrithi wa Petr Cech, pia wanamfuatilia kipa Stephane Ruffier wa St Etienne (Le 10).
Meneja wa Leicester City Craig Shakespeare amemuambia winga Riyad Mahrez , 26 anayehusishwa na kuhamia Arsenal kuwa hatocheza ikiwa haoneshi kujituma (Daily Telegraph).
Arsenal hawatomuuza Alexis Sanchez, 28, au Alex Oxlade-Chamberlain, 23, kwa timu yoyote ya EPL, licha ya kuwa wachezaji hao wanakaribia mwisho wa mikataba yao (Daily Star).
Alexis Sanchez ameiambia Arsenal kuwa anataka kuondoka na kwenda Manchester City. Makubaliano yamefikiwa kati ya Sanchez na City kwa pauni milioni 46.5, lakini Arsenal wanasita kumuuza kwa timu hasimu ya EPL, lakini huenda akaondoka bure mwisho wa msimu ujao (El Mercurio).
Crystal Palace wanataka kupanda dau kumtaka kipa wa Barcelona Jasper Cillesen, 28, (AS).
Paris Saint-Germain wanaongoza mbio za kumsajili Gareth Bale kutoka Real Madrid (Don Balon).
West Ham wamepunguza kasi ya kutaka kumsajili kipa wa Man City Joe Hart na sasa wanatafuta mshambuliaji (Sun).
Liverpool wanasema timu kadhaa zimemuulizia beki wake Mamadou Sakho, na wana uhakika kuna timu itaweza kulipa pauni milioni 30 (Liverpool Echo).
Mshambuliaji wa Man City Wilfried Bony anavutia timu kadhaa za China na City wana imani watapata pauni milioni 14 kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast (Independent).
No comments