Samatta Akabidhiwa Jezi Namba 10 KRC Genk
Mchezaji Wa
Kimataifa Kutoka Tanzania Anayekipiga katika
klabu ya KRC Genk ya
Ubelgiji Mbwana Samatta kuanzia msimu ujao atavaa jezi namba 10 katika kikosi
hicho akiachana na namba 77 aliyokuwa akiivaa tangu alipojiunga nao.
Samatta ambaye pia
ni nahodha wa Taifa Stars,
amekuwa akivaa jezi namba 10 pia katika kikosi cha timu ya taifa lakini tangu
alipojiunga na Genk mwaka jana amekuwa akivaa jezi namba 77.
Katika taarifa
iliyotolewa na Mtandao wa Genk, kuanzia msimu ujao Samatta atavaa jezi namba 10
ambayo awali ilikuwa ikivaliwa na kiungo mshambuliaji Tino- Sven Susic raia wa
Bosnia na Herzegovina.
Samatta alijiunga
na Genk akitokea TP Mazembe na hadi sasa ameichezea mechi 51 na kufunga mabao
17 na amekuwa mmoja kati ya wachezaji muhimu katika kikosi cha timu hiyo.
Msimu uliopita
aliiwezesha Genk kufika robo fainali ya Europa League wakitolewa na Celta de
Vigo katika hatua hiyo kwa mabao 4-3 ambapo katika mchezo wa kwanza ilifungwa
3-2 halafu ikatoka sare ya bao 1-1.
No comments