Header Ads

Miaka kumi ya ndoa bila kufanya tendo la ndoa




Wakati watu wengine ndani ya ndoa zao wanalalamika kuwa kadri miaka inavyozidi kwenda raha ya tendo la ndoa inazidi kupungua, wanandoa wawili nchini Australia ndio kwanza bado wanasubiri  muda ufike kuanza kufurahia tendo hilo.

James Na Michaela Reese ni wanandoa wa mda wa miaka 10 ambao hawajawahi kufanya tendo la ndoa hata mara moja.

Hali hii inatokana na mmoja wa wanandoa hao, Michaela kuwa na ugonjwa unaoitwa vaginismus ambao unasababisha misuli ya uke kukaza na kukakamaa sana hivyo kumfanya mwanamke apate maumivu makali sana wakati wa kufanya tendo la ndoa.

James anasema akiwa na miaka 14 aliamua kusubir mpaka atakapo funga ndoa ndio aanze kujihusisha na tendo la ndoa ,  na iliwachukua miezi 21 yeye na Michaela kusubiri ndoa yao hiyo ndipo wafanye tendo la ndoa lakini usiku wa ndoa yao mambo yalikuwa tofauti na ilishindikana kabisa kufanya tendo hilo

James aliamua kutunza viapo alivyokula wakati wa ndoa yao na amebaki kuwa mwaminifu kwa miaka 9 na mwezi december mwaka huu watakuwa wanakamilisha miaka 10 ya ndoa yao.

Je ingekuwa ni wewe ungeweza kuvumilia?
#Tafakari
Obby


No comments

Powered by Blogger.