Header Ads

Manchester United Yampiga Mtu 5 Marekani

Manchester United Wameanza Vyema Mechi Yao ya kwanza kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya baada ya Kuitungua timu ya zamani ya David Beckham, LA Galaxy 5-2

Ilichukua Dakika 2 Kwa Man United Kupachika Goli Lao La Kwanza Kupitia Kwa Marcus Rashford Baada Ya Kazi Nzuri kutoka Kwa Jesse Lingard, United Walisubiri mpaka Dakika Ya Ishirini Kuandika Goli La Pili Mfungaji Akiwa Rashford Pia Ambae Baadae Alipoteza Nafasi Nzuri  Sana Ya Kufunga Hat trick katika Mchezo Huo. 

Fellaini Alipachika Goli Maridadi Baada Ya Jesse Lingard Kufanya Kazi Nzuri Na Kumpenyezea Fellaini Ambaye Hakufanya Makosa Kuukwamisha Nyavuni Hivyo Kufanya Man United Kuongoza 3 Bila Kufikia Mwisho Wa Kipindi Cha Kwanza.
Image result for fellaini vs la galaxy 2017


Kipindi Cha Pili Kilianza Baada Ya Man United Kufanya Mabadiliko ya Kikosi Kizima, Kikosi Hiki Kilikuwa na wachezaji wapya Wa Man United Victor Lindelof Na Romelu Lukaku Alikosa Nafasi Nzuri Ya Kufunga Goli Lake La Kwanza Akiwa Manchester United Baada ya shuti lake Kuokolewa Na Mlinda Mlango Wa LA Galaxy. 
Image result for mkhitaryan vs la galaxy 2017


Manchester United Waliendeleza Ubabe Kipindi cha pili cha mchezo huo Kwa Kupachika magoli mawili zaidi kupitia Henrikh Mkhitaryan Na Anthony Martial
Image result for martial vs la galaxy 2017

Kuelekea Dakika Za Mwisho Mwisho Za Mchezo Timu Ya LA Galaxy Iliweza Kujipatia Goli 2 Kupitia Kwa Giovanni Dos Santos hivyo Kufanya Mchezo Kuisha 5-2
Image result for dos santos vs manchester united 2017

No comments

Powered by Blogger.