Header Ads

Majibu Ya Alikiba Kuhusu Collabo Zake Na Davido Pia Yvonne Chaka Chaka Yako Hapa

Kipindi cha nyuma kulikuwa na taarifa za Alikiba kufanya kolabo na Yvonne Chaka Chaka na Davido lakini hadi leo hazijatoka, sasa Alikiba amelizungumzia hilo.
Image result for alikiba yvonne chaka chaka

Alikiba na Yvonne Chaka Chaka
Muimbaji huyo wa Bongo Fleva ambaye December mwaka jana alionekana akiwa studio nchini Afrika Kusini na Yvonne Chaka Chaka, ameiambia XXL ya Clouds FM kuwa kazi na Mwana Mama huyo ilishafanyika ila kuna mipango inaweka sawa kwanza.
“Kiufupi kwamba nyimbo zipo na taratibu tulishafanya kama mlivyoona tupo studio lakini kuna ratiba lazima ziwepo sio tu umefanya halafu unatoa. Kuna mipango tupo nayo tayari na kila nyimbo itatoka kwa muda wake, na wimbo wangu unatoka hivi karibuni siwezi nikasema ni lini,” alisema Alikiba.
Kuhusu kolabo na Davido alisema, “unajua wasanii kama wasanii muda mwingine tunakuwa na maneno ya kuridhisha watu lakini kiukweli hakijafanyika chochote ila plan zipo za kufanya na muda tukiupata tutafanya il sijajua ni lini kwa sabau nyimbo nilizonazo ni nyingi sana,” alisisitiza.
Mwaka 2015 Davido aliwahi kuulizwa kuhusu na kolabo na Alikiba na jibu lake lilikuwa, “I have a song coming out with Alikiba too, that’s gonna be crazy”. Pia Nina Wimbo Nimefanya Na Alikiba Utatoka Utakuwa Mkali Sana

No comments

Powered by Blogger.