Header Ads

HAYA NDIO MAAJABU YA ALBUM MPYA YA JAY Z, 4:44

Zikiwa zimepita siku tano tangu album ya msanii nguli billionea wa marekana Sean Carter arimaarufu kama Jay Z kuanza mauzo ya album yake mpya ya 4:44 katika mtandao wake wa kuuza muziki, Tidal, album hiyo ishafanya maajabu katika mauzo.

Katika tweet ya Roc Nation ya hiv karibuni Jay Z alipongezwa kwa tweet iliyosomeka  “@S_C_ has earned 13 Platinum solo studio Album awards, more than any other hip-hop artist in @RIAA Gold & Platinum history. #RIAAPlatinum.

Album hiyo imefikia mauzo ya platnum kwa mujibu wa RIAA ndani ya siku 5 kumfanya Jay Z kuwa msanii mwenye album nyingi zenye mauzo ya platnum mpaka sasa kuliko msanii mwingine yoyote wa hip hop marekani. Mpaka kufikia album hii ya 4:44 Jay Z anafikisha studio album 13 zenye mauzo ya platnum

Kwa sasa album hii ya 4:44 inapatikana Tidal pekee lakini itaanza kupatikana spotfy na itunes kufikia ijumaa hii ya tarehe 7 july , na video ya wimbo wa 4:44 inapangwa kuachiwa mda wowote kuanzia sasa

No comments

Powered by Blogger.