Header Ads

Justin Bieber Apigwa marufuku china





Muimbaji  raia wa Canada, Justine Brown Bieber amezuiwa na serikali ya China kupitia mamlaka yautamaduni ya china (Beijing's culture buteau) kuingia nchini humo.

“Justin Bieber is a gifted singer, but he is also a controversial young foreign idol."  inasema taarifa ya mamlaka hiyo ikijibu maswali ya mashabiki wa bieber walikuwa wakihoji  kwanini hakuna tarehe inayoonesha show yoyote ya Bieber nchini humo katika ratiba ya dunia nzima ya album yake ya purpose kwa upande wa Asia (Asian leg purpose world tour)

"In order to maintain order in the Chinese market and purify the Chinese performance environment, it is not suitable to bring in badly behaved entertainers,” imeendelea  taarifa ya mamlaka hiyo.
“We hope that as Justin Bieber matures, he can continue to improve his own words and actions, and truly become a singer beloved by the public,”
Ingawaje haikutolewa sababu za moja kwa moja kwann zuio hilo limetolewa ama ni tabia mbaya zipi ambazo Bieber ameonesha mpaka kuzuiwa lakini wachunguzi wa mambo wanasema sababu zaweza kuwa ;

1. Bieber kuonekana kutokuwa na nidhamu baada ya video ikimuonyesha akitembea katika madhabahu ya Yasukuni jijini Tokyo, ambayo yalijengwa na Wajapan kwa heshima ya wanajeshi wake waliouawa vitani. Madhabahu hiyo kwa nchi ya China na Korea Kusini hutazamwa kama ishara ya dharau ya watu wa Japan na hawajajutia makosa yaliyotendwa na watawala wa nchi hiyo miaka ya nyuma.

2. Bieber kuonekana amebebwa na walinzi wake kuelekea ukuta maarufu wa china (The great wall of China) kitendo kinachosadikika kuonesha dharau.
Bieber hatakuwa msanii wa kwanza kuzuiwa kuingia china, kadhia hiyo ilimpata Jay Z, Bjork, Maroon 5 pamoja na Bob Daylan

China ina asilimia 57 ya vijana wanaozungumza kichina lakini wanapenda mziki unaoimbwa kwa kiingereza na kuhudhuria matamasha, ikilinganishwa na asilimia 51 ya wamarekani wanaohudhuria matamasha ya aina hiyo

No comments

Powered by Blogger.