Header Ads

BARAKA THE PRINCE KAWATOLEA MAPOVU MASHABIKI WANAODISS UAMUZI WAKE WAKUJITOA ROCKSTAR4000


Baada ya kujitoa RockStar Baraka da prince amesema hatakiwi mtu yeyote kumuingilia katika maamuzi yake kwasababu mwisho wa siku yeye ndiye hupiga kazi na anajua nini ambacho amekilenga .
Muimbaji huyo wa bongo fleva amesema hayo mara baada ya mashabiki kumtolea povu kutokana na maamuzi ambayo ameyafanya ya kujitoa katika management yake .

"Hii ni biashara yangu mtu atakayekuja ku'complain eti kwanini Barakah kajitoa RockStar iyo ijue haikuhusu kwasababu inanihusu mimi na RockStar wewe kama shabiki deal na muziki tu yani personal life na personal business ya kwangu haikuhusu inabidi u'deal na vitu vingine na sometimes unajua hutakiwi kuangalia mtu anasema nini katika maisha yako au nani ataongea nini fanya kile ambacho unahisi ni maamuzi mazuri na yenye faida kwako kwanini ukae unang'ang'ania watu kukusifia kwa nothing au kwa kitu ambacho hakipo...we msanii mkali, hadi lini? Sihitaji hiyo mimi nataka kufika sehemu na mipango yangu mimi ujue mpaka nasaini mkataba na RockStar na kufanya nao kazi which means nilikuwa na mipango yangu kwahiyo nikiona mipango yangu haiendi kama nilivyotegemea naruhusiwa ku'move on na kuendelea na ratiba zingine" alisema Baraka the prince.

"hatakiwi mtu yeyote ku'complain kwasababu ni maamuzi yangu na pia hata nikifeli ni kwa hasara yangu nikifaulu pia ni kwa faida yangu na familia yangu kwahiyo mtu atakaye-complain kwanini Barakah kajitoa RockStar mimi nahisi atakuwa na mapungufu sana itabidi ajiangalie kwanini yani uingilie life ya mtu personal na mimi ndio najua nateseka kiasi gani"aliongeza .

Katika upande mwingine Barakah ameishukuru Record label hiyo mahali ambapo imemfikisha na kusema kuwa hata kama ameondoka RockStar bado itabaki katika historia ya maisha yake .

"Chochote kile ambacho wamekifanya kwangu Rockstar kina manufaa kwasababu target yao ni manufaa wameplay part yao kwa uwezo wao hata kama nitakuwa nani tayari wapo katika historia yangu kwahiyo ni watu ambao siwezi kusahau pale ambapo wamenisupport kutoka ngazi moja kwenda ngazi nyingine" a

No comments

Powered by Blogger.