Header Ads

Alexandre Lacazette Akamilisha Vipimo Vya Afya Arsenal

Mshambuliaji wa Lyon Alexandre Lacazette amekamilisha vipimo vya afya kabla ya kujiunga na Arsenal kwa kitita cha rekodi ya pauni milioni 45.
Image result for lacazette
The Gunners ilikuwa imetoa kitita cha chini lakini kikakataliwa na hivyobasi kuendelea na mazungumzo.
Kitita hicho ambacho Kinatarajiwa Kufika  hadi paundi milioni 52 kitapita kile alichonunuliwa Mesut Ozil kutoka Real Madrid cha paundi milioni 42.4 Mwaka 2013.
Lazazette alikuwa wa pili kwa idadi ya mabao katika ligue Msimu uliopita akiwa na mabao 28.
Amefunga mabao 129 katika mechi 275 katika mashindano yote tangu alipoanza kuchezeshwa katika timu kikosi cha kwanza 2009-10.
Edison Cavani Pekee Ndo Alimzidi Lacazette Msimu Uliopita  aliyefunga mbao 35.
Lacazzette ambaye ameichezea Ufaransa mara 11 amehusishwa na vilabu kadhaa vikuu na alitarajiwa kujiunga na Atletico Madrid.
Wiki iliopita mkurugenzi mkuu wa Arsenal Iva Gazidis aliahidi kuwasajili wachezaji wa kiwango cha juu wakati wa mahojiano na wanahabari.
Arsenal kufikia sasa imemsajili beki wa kushoto Sead Kolasinac, ambaye alijiunga na klabu hiyo kutoka Schalke.

No comments

Powered by Blogger.