Tetesi Za Usajili Barani Ulaya
Liverpool wamemuulizia winga wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain, 23, ambaye huenda akagharimu pauni milioni 25, huku Manchester City na Chelsea pia wakimnyatia (Mirror).
Manchester City wana uhakika wa kumsajili beki kutoka Brazil anayechezea Juventus Dani Alves wiki hii. Chelsea na Tottenham pia wanamtaka Alves (Sun).
Manchester City wana matumaini ya kukamilisha usajili wa mabeki watatu kabla ya kwenda Marekani mwezi ujao kwa ajili ya mechi za kujiandaa na msimu mpya. Miongoni mwao wanatarajia kufanikisha uhamisho wa Dani Alves na Kyle Walker (Daily Mail)
Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Ousmane Dembele, amekutana na meneja wa Manchester City Pep Guardiola, kuzungumzia uwezekano wa kuhamia Etihad (Le 10 Foot).
Atletico Madrid wanafikiria kumchukua Zlatan Ibrahimovic (Tuttosport).
Meneja wa Chelsea Antonio Conte anafikiria kumchukua winga wa Sevilla, Vitolo, 27, kwa pauni milioni 35 (Daily Mirror).
Manchester United wana uhakika wa kumsajili kiungo wa Chelsea Nemanja Matic, 28, wiki hii kwa takriban pauni milioni 40. Hata hivyo Jose Mourinho alikuwa akimtaka zaidi Eric Dier au Radja Nainggolan Wa AS Roma kabla ya Matic (Telegraph).
Inter Milan wamewaambia Manchester United watoe pauni milioni 44 kama wanamtaka Ivan Perisic (Gazzetta dello Sport).
Mshambuliaji Naby Keita anayesakwa na Liverpool hatoruhusiwa kuondoka Leipzig bila malipo yasiyopungua pauni milioni 70 (Guardian).
Leicester City watalazimika kulipa takriban pauni milioni 40 iwapo wanataka kumsajili kiungo mshambuliaji wa Swansea Gylfi Sigurdsson, 27 (Leicester Mercury).
West ham wanajiandaa kuvunja rekodi yao ya usajili kwa kulipa zaidi ya pauni milioni 20 kumchukua mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud, 30 (Telegraph).
West Ham wapo tayari kulipa pauni milioni 50 kuwachukua Theo Walcott na Olivier Giroud kutoka Arsenal (Daily Star).
West Ham pia wanamtaka mshambuliaji wa Sampdoria, Luis Muriel, 26 (Sun).
AC Milan wamemfanya beki wa kati wa Arsenal Laurent Koscielny, kuwa kipaumbele cha usajili, wakati klabu hiyo ya Seria A ikitaka kuimarisha safu yake ya ulinzi (Telefoot).
Lyon wameacha kumfuatilia Olivier Giroud, huku rais wa klabu hiyo akidai kuwa Arsenal hawataki kumuuza (Evening Standard).
Tottenham wameambiwa watahitajika kulipa pauni milioni 26 ili kumsajili kiungo Adrien Silva, 28, kutoka Sporting Lisbon ya Ureno (Record).
Kiungo mshambuliaji wa Leicester City Riyad Mahrez, 26, anafikiria kusaini mkataba wa miaka minne ambao amepewa na Arsenal, baada ya kuchoka kuwasubiri Barcelona (Sport).
Kiungo mshambuliaji wa Real Madrid, James Rodriguez, 25, anayesakwa na Manchester United huenda akabakia Spain, ikiwa Cristiano Ronaldo, 32, ataondoka (Don Balon).
Trabzonspor ya Uturuki inazungumza na Liverpool kuhusu usajili wa Lucas Leiva, 30 (Fotomac).
Barcelona wanazungumza na kiungo wa zamani wa Tottenham, Paulinho, 28, anayechezea Guangzhou Evergrande (Sky Sports).
Barcelona watamtaka tu Paulinho iwapo watashindwa kumsajili Marco Verratti, 24, kutoka PSG (Daily Mail).
Beki wa Manchester City Aleksander Kolarov, 31, amesema siku moja anataka kurejea katika klabu yake ya zamani, Lazio (Il Messaggero).
No comments