Header Ads

Ryan Giggs -Wayne Rooney Anaweza Kuendelea Kucheza Manchester United

Aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Wales na klabu ya Manchester United, Ryan Joseph Giggs amesema, "Wayne Rooney ataweza kusalia katika kikosi cha United endapo atakubaliana na masharti ya kutochezeshwa kila mchezo utakao ikabili timu hiyo".

Giggs: Rooney could stay at Manchester United

Wayne Rooney Amejikuta Akitumia Muda Mwingi kukaa benchi katika msimu wa mwaka 2016/17 chini ya kocha Jose Mourinho, Licha Ya Kuwa Nahodha Pia Mfungaji Bora Wa Muda Wote Wa Klabu Hiyo Ya Jiji La Manchester.

Wayne Rooney Alifanikiwa Kuanza Michezo 15 Na Kufunga Magoli 5 Msimu Huu Kwenye Ligi Kuu Ya Uingereza

"Wayne Rooney Ni Mfungaji Mahiri Ukimpa Nafasi Tu Ni Lazima Atafunga Magoli" Alisema Ryan Giggs

"Kama Atakubaliana Na Kutokuwa Chaguo La Kwanza Ama Kama Ataweza Kuboresha Uchezaji Wake Kitu Ambacho Nilifanya Nilipokuwa Na Umri Sawa Na Wake, Asiwe Na Uhakika Wa Kucheza Kila Mechi Ila Akacheza Michezo 25-30 Na Kuonyesha Mchango Wake Kwenye Michezo Hiyo. Kama Ataweza Kufanya Hivyo Sidhani Kama Ataondoka Man United"

Wayne Rooney alikaririwa akisema kuwa angeamua hatima yake baada ya kumalizika kwa ligi kuu nchini Uingereza lakini mpaka sasa mchezaji huyo ameshindwa kuonyesha dalili yoyote ya kuondoka United.

No comments

Powered by Blogger.