Header Ads

Jux Na Vanessa Mdee huwa Nawaona Pamoja - Mimi Mars

Msanii wa Bongo Fleva, Mimi Mars ambaye ni mdogo wake Vanessa Mdee amezungumzia taarifa za kuachana kati ya dada yake na Jux.



Mimi Mars alisema hawezi kujua kama kweli wameachana ila bado anawaona pamoja.
“Unajua bado wanawasiliana, wanaongea kwa hiyo sielewi, (mambo ya mapenzi) kuna kuachana, kuna kurudiana kwa hiyo hatuwezi kujua hicho kitu kilichokuwa kinapita hapo katikati kilikuwa nini,” Mimi Mars alisema hayo kwenye kipindi cha Twenzetu cha Times FM.
Nje Na Hilo Mwana dada Huyo Aliulizwa kama anadate na msanii yeyote Wa Bongo Fleva au Kama alishawahi kufikiria kufanya hivyo ili kupanda kimuziki, Mimi Mars alijibu, “hapana kabisa, kuzushiwa nimezushiwa lakini sijawahi kuwa na mtu kwenye Bongo Fleva”.
“Kwangu mimi ni kitu ambacho nisingetaka kufanya, so sijui kama ingenishusha au kunipandisha, ni kitu ambacho hakipo katika dictionary yangu,” alisema Mimi Mars
Muimbaji huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya unaokwenda kwa Jina La ‘Dedee

No comments

Powered by Blogger.