Header Ads

FLORENTINO PEREZ : MTU WA PESA Aliyeasisi matumizi makubwa ya pesa katika soka

Florentino Eduardo Pérez
Rodríguez,

Alizaliwa March 8, 1947 (ana miaka 70)

Katika jiji la Madrid, nchini Uhispania.

Papa Perez kama wanavyomuita ni mfanya Biashara msomi aliyekuja kubadilisha mtazamo wa matumizi ya Pesa katika mpira.

Alianzisha mfumo mpya wa kipesa uliofahamika kama "los galacticos"
Ingawa Haikua rahisi.

Alijitambulisha kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1995 alipogombea katika ngazi hiyo ya juu kabisa katika klabu ya real madrid.

Perez alipinga vikali mfumo mbovu wa kifedha klabuni hapo lakini alibwagwa na Remon Mendoza kwa zaidi ya kura 699
Katika uchaguzi uliofanyika Tarehe 19 February.

Mtaalam huyo wa ujenzi ambae ni mhitimu wa Chuo kikuu cha polytechnic university of Madrid.
Aliamua kurudi tena katika mbio za kuwania urais wa real Madrid na safari hii akichuana na Lorenzo Sanz, katika uchaguzi mgumu kuwahi kutokea Sanz akichagizwa na ushindi wa makombe mfululizo katika utawala wake huku perez akishikilia msimamo wake wa matumizi ya fedha ambapo ilimlazimu ahaidi kumleta Luis Figo, jambo ambalo lilionekana la kushangaza kama litatokea na hapo ndipo alipoaminiwa ili kuona kama itatokea , na kumpelekea kushinda uchaguzi huo.

Na hapo ndipo ulipokua mwanzo "Mr.Crazy Transfer Fees"
Akianza kutimiza ahadi yake kumpeleka Figo katika dimba la Santiago Bernabeu kutoka katika mikono ya wapinzani wao wa jadi Barcelona na jambo hili lilimfanya Perez akose mshindani katika chaguzi ya Mwaka 2004 ambapo alipata ushindi wa 94%

Perez alikuja kupumzika nafasi ya urais Mwaka 2006 na baadae kugombea tena 2009 ambapo alishinda na kuendeleza mfumo wake wa utumbuaji wa Pesa kuwajaza wachezaji hodari katika himaya yake
Hii iliifanya Madrid kuwa timu ya kuogopwa zaidi ikitisha uwanjani na sokoni,

Perez alisuka mifumo imara ya Pesa kuiwezesha klabu hiyo kujiendesha.
Akiwa na utajiri wa zaidi ya shilingi za kitanzania trillion 5,

Perez ambae mkewe Bi.Maria Angeles alifariki Mwaka 2012 wakiwa wamepata watoto watatu, Pia ni rais wa Wajenzi nchini humo,
Ameshinda jumla mataji 31  tangu aanze kuiongoza klabu hiyo

3 La Liga
2 FIFA Club World Cup
2 Copa del Rey
3 Spanish Super Cup
3 Champions League
1 Intercontinental Cup
3 European Super Cup
1 Basketball European Cup
1 Basketball Intercontinental Cup
4 Basketball League
5 Basketball Copa del Rey
3 Basketball Spanish Super Cup

No comments

Powered by Blogger.