Header Ads

MICHANGO YA HISANI YAUA WAZIRI

 Waziri wa Afya, Slim Chaker wa nchini Tunisia, amefariki dunia baada ya kupata mshtuko wa moyo aliposhiriki mbio za kuchangisha fedha za kupambana na saratani. .

Waziri huyo mwenye umri wa miaka 56, aliugua baada ya kukimbia mita 500 katika mji wa Nabeul.

Mbio hizo zilikuwa na lengo la kukusanya michango kwa ajili ya ujenzi wa kliniki ya watoto wenye kansa.

Slim Chaker alikimbizwa hospitali iliyopo Mjini Tunis baada ya kupata shambulio hilo la moyo
na kufariki akiwa anatibiwa hospitalini hapo.

No comments

Powered by Blogger.