Header Ads

TUPAC HAJAFA; SUGE KNIGHT

Miaka 21 ya kifo cha Tupac Shakur, mengi yamesikika lakini hili ni kubwa zaidi.

Hii ni kutoka kwenye kinywa cha Mtayarishaji wa muziki na mtu wa karibu sana rapa Tupac Shakur, SUGE KNIGHT ambaye amekiri kuwa anaamini rapa Tupac anaweza kuwa hai.

Akizungumza kwa njia ya simu na Ice -T pamoja na Soledad O'Brien, huku akiwa jela mjini Los Angeles, Suge alisikika Live kwenye Clip ambayo ni Teaser ya ujio wa kipindi kipya, "Who Shot Biggie and Tupac? ambacho kitaruka Jumapili hii kupitia Fox Televisheni.

Moja ya sababu kuu anazoziamini ni anakumbuka siku anaondoka hospitali, alimuacha #Tupac mzima wa afya huku wakicheka na kutaniana,
“I mean, when I left that hospital, me and Pac were laughing and joking."- alisisitiza #SugeKnight

Bomu lililupuka pale Suge alipoulizwa kuwa anafikiri Tupac anaweza kuwa hai? Suge alijibu, Nitakwambia nikiwa pamoja naye, Huwezi jua.

Cheki na Video hiyo hapo juu, kisha niachie comment yako kwa chochote.

No comments

Powered by Blogger.