Header Ads

Rapa B.o.B ataka kuthibitisha iwapo dunia ni duara


Mwanamuziki wa Marekani wa mtindo wa rap B.o.B. anatafuta msaada wa kutuma satelaiti kuthibitisha iwapo kweli dunia ni duara.

Rapa huyo ambaye jina lake halisi ni Bobby Ray Simmons Jr, ni mmojawapo ya watu wanaoamini kwamba dunia ni kama sahani na sio duara.
Baadhi ya wanaomini kuwa dunia ina umbo la sahani wanaodaia wafanyakazi wa NASA shirika la wana anga za juu wanalinda ukingo wa dunia kuzuia watu wasianguke. Anajaribu kuchangisha $200,000 katika mtandao wa kuchangisha fedha wa GoFundMe na mpaka sasa amefanikiwa kukusanya kima cha $650, lakin kampeni hiyo imekuwa ikizungumziwa kwamapana katika mtadao huo.alisema
'Nionyeshe upinde'
"Nimeanzisha kampeni hii kwasababu ningependa kutuma kama sio satelaiti moja basi nyingi katika anga za juu kujaribu kutafuta upinde unaoifanya dunia kuwa duara," alisema katika video iliowekwa kwenye mtandao huo.
"Nautafuta upinde," ameongeza B.o.B


No comments

Powered by Blogger.