MFALME MSWATI WA III AOA MKE WA 14
MFALME Mswati wa Tatu wa Swaziland kwa mara nyingine
ameongeza idadi ya wanawake kwa kuoa mwanamke mwingine. Katika kuadhimisha
Ngoma ya Umhlanga ambayo hufanyika kila mwaka kwa kumpa mfalme fursa ya
kuchagua mwanamke wa kuoa, mfalme huyo hivi karibuni alimchagua Siphele mwenye umri wa miaka 19 kuwa mkewe wa 14.
Msichana huyo ambaye ni binti wa waziri Jabulile Mashwama
katika serikali ya nchi hiyo, alipewa manyoya maalum mekundu ya ndege
anayejulikana kama emagwalagwala ambaye huhusishwa na sherehe hiyo maalum ya
kifalme. Mswati ambaye ana umri wa miaka 49 huchagua wanawake waliovuka umri wa
miaka 19.
Wakiwa kwenye sherehe za mavuno.
Pamoja na talaka kupigwa marufuku katika nchi hiyo ya
kifalme, Mfalme Mswati amewahi kuwataliki wake zake watatu. Siphele ambaye ni
mhitimu wa Waterford Kamhlaba World University College, alifuatana na Mfalme
Mswati alipohudhuria Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa hivi karibuni.
Habari hiyo ilifichuliwa na msimamizi wa sherehe za kifalme,
Hlangabeza Mdluli, aliyethibitisha kwamba Mswati alikuwa amefuatana na mkewe
huyo ambaye kwa umri ndiye mdogo zaidi.
Wake wengine wa Mswati
Wake zake wengine ni pamoja na: Inkhosikati LaMatsebula,
Inkhosikati LaMotsa, Inkhosikati LaMbikiza, Inkhosikati LaNgangaza, Inkosikati
LaMagwaza (ameachika), Inkhosikati LaHoala (ameachika), Inkhosikati LaMasango,
Inkhosikati LaGija (ameachika).
Wengine ni: Inkhosikati Magongo, Inkhosikati LaMahlangu,
Inkhosikati LaNtentesa, Inkhosikati LaNkambule, Inkhosikati Ladube na
Inkhosikati LaFogiyane. Mfalme King Mswati, anayejulikana pia kama Ngwenyama,
yaani simba, anasemekana kuwa na watoto zaidi ya 13 ambao ni pamoja na binti
yake mkubwa zaidi aitwaye Sikhanyiso, Sibahle Dlamini, Makhosothando Dlamini,
Majaha Dlamini, na Tiyandza Dlamini.
Wengine ni Sakhizwe Dlamini, Saziwangaye Dlamini, Bandzile
Dlamini, Lindaninkosi Dlamini, Mcwasho Dlamini, Temtsimba Dlamini na Temaswati
Dlamini, among others. Baba yake Mswati, Mfalme Sobhuza wa Pili, alioa wanawake
70. Mswati amekuwa akishutumiwa kwa kujilimbikizia utajiri wakati watu wake
wengi ni maskini.
Hivi karibuni, nchi hiyo ndogo ilitumia kiasi cha Dola
milioni 2.2 (sawa na Sh. bilioni 5) kwa kununua magari ya anasa aina ya BMW
740i na pikipiki 80. Magari hayo yalikuwa ni kwa ajili ya viongozi wa Jumuia ya
Maendeleo Kusini mwa Afrikca (SADC) waliyoyatumia kwa ajili ya mkutano wa siku
mbili.
No comments