Header Ads

Tyga Amjia Juu Rob Kardashian

Rapper Tyga amemtaka Rob Kardashian kutomuhusisha mtoto wake [King Cairo Stevenson] mwenye miaka mitano katika ugomvi alionao na mpenzi wake Blac Chyna.
Tyga aliwahi kuwa na mahusiano na Chyna kwa zaidi ya miaka mitatu na kufanikiwa kupata mtoto huyo mmoja.
Hivi karibuni kumeonekana kuwa na mgogoro mkubwa kati ya Rob pamoja na mpenzi wake Blac Chyna, huku kijna huyo kutoka katika familia ya Kardashian akimtuhumu mwanamitindo huyo ambaye amezaa naye mtoto mmoja kuwa amekuwa akimsaliti katika mahusiano yao ambayo yamedumu kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Hivi Karibuni Rob alifululiza kumshushia mvua ya matusi Blac Chyna huku akiweka picha za utupu za mrembo huyo kwenye mitandao ya kijamii, jambo ambalo mtandao wa Instagram ukalazimika kuifuta akaunti ya kijana huyo.

No comments

Powered by Blogger.