Tetesi Za Usajili Barani Ulaya
Mshambuliaji wa Uhispania na Chelsea Diego Costa, 28, anataka kuondoka Stamford Bridge kwa wakati anaotaka yeye, na jambo hilo linachelewesha hatua ya Chelsea kumsajili Romelu Lukaku, 24, kutoka Everton (Daily Mirror).
Antonio Conte anataka Chelsea watoe hata pauni milioni 100 kumsajili Romelu Lukaku, kama Everton wanataka kiasi hicho ili kumuuza (The Telegraph).
Mshambuliaji kutoka Argentina Lionel Messi, 30, atasaini mkataba mpya Barcelona mara tu atakaporejea kutoka kwenye fungate yake baadaye mwezi huu (Goal).
Paris Saint-Germain wanajiandaa kupanda dau jipya la kumtaka mshambuliaji wa Monaco Kylian Mbappe, 18, na wamewasiliana na wawakilishi wa mchezaji huyo (L'Equipe).
Arsenal wanapanga kutoa pauni milioni 70 kuwasajili viungo wawili kutoka Sporting Lisbon ya Ureno, William Carvahlo, 25, na Gelson Martins, 22 (A Bola).
Arsene Wenger atakutana na Alexis Sanchez, 28, na Hector Bellerin, 22, wiki hii kujaribu kuwashawishi wasiondoke Emirates (The Sun).
Everton wana uhakika wa kumrejesha Goodison Park Wayne Rooney, 31, kutoka Manchester United msimu huu (TalkSport).
West Ham United wanataka kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Javier Hernandez "Chicharito" , 29, kutoka Bayer Leverkusen (Telegraph)
Liverpool wanapanga kutoa euro milioni 12 kumsajili kipa wa Sevilla Sergio Rico (ABC Sevilla).
Chelsea wameonesha dalili kuwa wapo tayari kutoa pauni milioni 60 kumsajili beki wa kushoto Alex Sandro kutoka Juventus (Telegraph).
Barcelona wanaongoza katika mbio za kumsajili beki wa Juventus Leonardo Bonucci. Chelsea wanataka kumsajili beki huyo, lakini yeye angependa kwenda Barcelona (Daily Mirror).
Inter Milan wanataka kupanda dau la kumtaka mshambuliaji wa PSG Angel di Maria (Tuttosport).
Kipa wa zamani wa Arsenal Jens Lehmann anatarajia kurejea Emirates kama mmoja wa makocha wa kikosi cha kwanza (Guardian).
Gianluigi Donnarumma amekataa kuhamia Paris-Saint-Germain na amekubali kusaini mkataba mpya kusalia AC Milan (Sky Sport Italia).
Kiungo wa zamani wa Manchester United Ravel Morrison, 24, amefanya mazoezi na Birmingham City, akitaka kuhamia klabu hiyo kutoka Lazio (Daily Mirror).
Southampton wanataka kukamilisha usajili wa pauni milioni 8.75 wa mshambuliaji Yann Karamoh, 18, ambaye ana mzozo na klabu yake ya Caen ya Ufaransa (Sun).
Meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone ameanza mazungumzo na klabu hiyo kuhusu mkataba mpya utakaompeleka hadi mwaka 2020 (AS).
Meneja wa Manchester United Jose Mpurinho anakasirishwa na hatua ya klabu hiyo kutosajili wachezaji zaidi ya Victor Lindelof, 22, peke yake mpaka sasa (Daily Mirror).
Jose Mourinho anataka mshambuliaji Alvaro Morata, 24, kutoka Real Madrid na kiungo Nemanja Matic, 28, kutoka Chelsea wajiunge na kikosi chake kabla ya Jumapili watakapoanza safari ya Marekani ya mechi za maandalizi (Daily Star).
Real Madrid 'wamekomaa' na Alvaro Morata hadi Manchester United watakapotoa pauni milioni 79 (Marca).
Kiungo kutoka Guinea Naby Keita, 22, anataka kuhamia Liverpool, lakini klabu yake RB Leipzig inataka pauni milioni 70 (Daily Mirror).
Crystal Palace wameshindwa kulipa pauni milioni 30 wanazotaka Liverpool kwa ajili ya beki wa kati Mamadou Sakho, 27 (Guardian).
Manchester United wanajiandaa kupanda dau kumsajili beki Marc Bartra, 26, kutoka Borussia Dortmund (Manchester Evening News).
Newcastle bado hawajafanikiwa kumsajili kipa Pepe Reina, 34, kwa kuwa Napoli hawajapata mtu wa kuziba nafasi yake (Newcastle Chronicle).
Leicester City wamefanya mazungumzo ya awali na Sevilla kuhusu usajili wa kiungo Vicente Iborra (Sky Sports).
Kipa Wojciech Szczesny amerejea Arsenal kutoka Roma alipokuwa kwa mkopo kwa miaka mwili (Instagram).
No comments