Tetesi Za Usajili Barani Ulaya
Arsenal wanajiandaa kutoa pauni milioni 125 ili kumsajili Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco na kuwazidi kete Real Madrid (Sunday Mirror).
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amemuambia Alexis Sanchez, 28, kuwa hatojiunga na Manchester City msimu huu (Mail on Sunday).
Everton wanapanga kutaka kutoa pauni milioni 20 kumsajili mshambuliaji wa Arsnenal Olivier Giroud, 30 (The Sun).
Meneja wa Bayern Munich Carlo Ancelotti ameonekana kutaka klabu yake kumsajili Alexis Sanchez kutoka Arsenal kwa kusema Sanchez ni "mchezaji mzuri" (London Evening Standard).
Manchester City pia wanamtaka Alexis Sanchez, lakini Arsenal hawatoruhusu mchezaji huyo kwenda katika klabu hasimu inayocheza Ligi Kuu ya England (Mail on Sunday).
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola, yuko tayari kumruhusu kipa Joe Hart , 30, kuhamia kwa mahasimu wao Manchester United (Sunday Express).
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho bado atataka kumsajili mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku, 24, hata kama klabu hiyo itamsajili Alvaro Morata, 24, kutoka Real Madrid (Sun).
Jurgen Klopp atamzuia Daniel Sturridge, 27, kuondoka Liverpool, kwa sababu itagharimu sana kupata mtu wa kuziba nafasi yake (Mirror).
Kiungo wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain, 23, amekataa kusaini mkataba mpya Arsenal na yuko tayari kumaliza mkataba wake wa sasa na kuwa mchezaji huru msimu wa mwakani (Sunday Times).
Mshambuliaji Diego Costa, 28, anakaribia kujiunga tena na Atletico Madrid kutoka Chelsea, lakini hatoweza kucheza mpaka mwezi Januari (AS).
Beki wa Roma Anonio Rudiger, 24, ameonesha dalili kuwa anajiandaa kujiunga na Chelsea katika picha aliyoweka kwenye Instagram (Metro).
Chelsea wanataka kumsajili beki wa Exeter City Ethan Ampadu, 16, na wanajadili fidia kwa klabu hiyo ya daraja la pili (Guardian).
Swansea wanakaribia kumsajili kiungo mchezeshaji wa Las Palmas Roque Mesa, 28, kwa pauni milioni 11 (Sunday Telegraph).
Wakala wa beki wa kulia wa Arsenal Hector Bellerin, 22, wameanza mazungumzo na Barcelona ya kumrejesha mchezaji huyo katika klabu yake ya zamani (Sport).
Beki wa Leeds United Charlie Taylor, 23, anakaribia kujiunga na Burnley (Yorkshire Post).
No comments