Header Ads

Kaa Tayari Kwa Ujio Wa Wasanii Kutoka Kwenye Lebo Ya Alikiba Na Bidhaa Zake

Miezi Kadhaa Baada Ya KingKiba Kudokeza Kuhusu Ujio Wa Bidhaa Zake Sokoni, Hatimae Kiba Kaweka Wazi Zaidi Kuhusu Mchakato Mzima Unavyoenda Hivyo Basi Tegemea kuona bidhaa za mavazi na vinywaji kutoka kwa msanii huyo.


Alikiba amethibitisha hayo wakati alipokuwa akiongea na mtangazaji wa kipindi cha Msetoea cha Citizen Radio, Mzazi Willy Tuva.
“Kulikuwa na tetesi hizo kuwa Alikiba ataingiza bidhaa zake sokoni lini, lakini kiukweli ipo ni kwamba tofauti na watu wengi walivyokuwa wakifikiria lakini hizo bidhaa zipo, nimeshasajili kila kitu kwa hiyo ni kuingiza tu bidhaa,” alisema Kiba.
“Plan zetu ndio zinafanyika na soon watu tutawaonyesha kuanzia chini ni kitu gani ambacho tunakifanya ili twende nao sambamba wajue bidhaa itafika lini au kama imekamilika tuwaonyesha kama imekamilika. Kila kitu nitakjuwa nawaonyesha kama ni energy drinks, mavazi,” aliongeza.


Muimbaji huyo aliendelea kwa kuzungumzia kuhusu mipango yake ya kufungua lebo kama baadhi ya wasanii wengine wakubwa, amesema, “Mimi nilisha kuwa na lebo muda mrefu sana, sema kazi zangu hazikuwa za matangazo kama hivyo. Ni muda mrefu nimeanza kufanya muziki na kusaidia watu sio leo, toka nipo katika game kabla sijapumzika nilikuwa na lebo yangu ya muziki lakini haikuwa inatangazwa. Sasa hivi kila kitu kipo kwenye utandawazi, kila mtu anatakiwa kujua Alikiba ana lebo na anafanya hivi na hivi.”
“Nipo na wasanii ambao nimewasaini lakini bado sija watangaza wala kutoa kazi zao, tupo kwenye process za mwisho kwa sababu kila mtu kasharekodi nyimbo zake bado kushoot video ndio tuwatangazie watu,” alisisitiza.

No comments

Powered by Blogger.