Header Ads

FAHAMU KUHUSU BOMU LA NUCLEAR

Bomu la nyuklia hutengenezwa kutokana na madini yenye asili ya Radioactive kama vile Uraninum au Plutonium. Madini haya yana tabia kuwa yakistuliwa kidogo tu basi yanaanza process inayoitwa nuclear fission ambapo hupasuka vipande vidogo vidogo huku yakiwa yaanaachia joto jingi sana. Madini ya uranium yana mifumo (isotopes) mbili, Uranium U-235 na Uranium U-238. Mfumo wenye nguvu za nuklia ni ule wa U-235, hata hivyo madini ya uranium ya asili kama yanayochimbwa hapa kwetu yana kama nusu asilimia tu ya U235, wakati asilimia karibu 99.5 ni U-238. Bomu moja la Nyukilia huhitaji U-235 kama kilo hamsini hivi hivi, kwa hiyo ili kuzipata hizo kilo hamsini inabidi uwe na uranium asili zaidi ya tani mia moja halafu uichuje kwa kutumia chekecheo ziitwazo centrifuge ili kuondoa U-238 ambayo ni nzito kidogo na kuacha U235 ambayo ni nyepesi. Kuchuja tani moja ya Uraniuma inaweza kuchukua miaka miwili au hata mitano kutegemea na ubora wa centrifuge ulizo nazo.Ukishaweka iliyochujwa mahali palipotulia, unachohitaji ni kuidisurtb kidogo tu hata kwa kuiangushia mchanga, halafu yenyewe inaaza nuclear fission inayosababisha kitu kinaitwa chain reaction ambayo hutoa joto kali sana na kuunguza kila kilicho hapo katika maeneo yake. Nguvu za nuklia hutumia joto hilo badala ya makaa ya mawe kuchemsha maji kutoa mvuke wa kuendesha mashine za hiyo.


No comments

Powered by Blogger.